1. Ghostwriter
Kama unafikria kuandika kitabu lakini huna muda wa kuandika kitabu hicho au unajua jambo fulani au hadithi fulani lakini kuandika sio kitu unachopendelea kuna watu au makampuni mengi yanayofanya kazi hiyo (ghostwriters). Ila ni ghali sana. Hivyo kama unataka unaweza kuwapata guru.com.
2. Copy editing and Proofreading
Kama umeshaandika kitabu hivyo unachohitaji ni watu wa kukisahihisha kitabu chako.
a) Editor wa kuangalia makosa ya maneno tu. Ingawaje kuna spell checking lakini kumbuka kuna maneno yanafanana hata artificial intelligence haiwezi kuyagundua mfano unataka kuandika mad lakini ukaandika mud. Mtu akisoma ndio ataelewa umekosea.
b) Editor wa kuangalia grammar mistakes. Ukweli ni kuwa always a second set of eyes is very important katika kuandika kitabu. Hata kama unaandika kitabu kwa lugha ya kiswahili ni muhimu sana kupata mtu wa kufanyia hii kazi.
c) Editor ambao wanakubadilishia maneno katika habari yako ili ilete maana zaidi kwa wasomaji au ipendeze. Sasa hao watu ni muhimu pia kuwatumia lakini inategemea na kitabu unachoandika.
3. Book Tittle
Baada ya kumaliza kitabu chako natumaini utakua na jina tayari au ukimpa editor anaweza kukushauri kitabu chako ukipe jina gani. Au watu unaowafahamu pia waulize.
4. Book Cover
5. ISBN -International Standard Book Number
Hii ni unique number kila kiyabu kinacho. Kuna website kama Kindle ebook publishing wanakupa number zao lakini ni bora ununue ambayo itaweza kutumika katika sehemu mbalimbali & international. Investment ya hii number ni muhimu sana. Ila kumbuka kila format ya kitabu inatumia ISBN moja. Kama unataka kuchapisha kitabu chako kwa format ya paperback, ebook na audio ni lazima uwe na hizi ISBN 3 etc. Na pia kama ukiandika 2nd edition ya kitabu chako ni lazima utumie namber nyingine siyo hiyo hiyo tena.
ISBN moja + Barcode ni $150 lakini ukinunua 10 ISBN + 10 Barcodes unalipa $320 tu. Hizi ISBN unaweza kuzitumia kwa miaka 100 au kurithisha ndugu zako kama hutatumia.
6. Marketing
Jinsi ya kukitangaza kitabu chako ni wewe upendanyo au kwa uwezo wako. Hivyo kujua kitabu chako soko lake ni lipi, wana umri gani, elimu gani, income yao ni kiasi gani ni muhimu ili usije ukapoteza muda wako na hela yako kukitangaza kwa watu ambao hawatanunua kitabu chako.
7. Distribution Channels
Hizi ni sehemu unazotaka kuuza vitabu vyako. Hii inategemea na wateja wako au kitabu chako. Kuna vitabu vingine watu wanataka kuwa nacho hard copy ama kumbukumbu na kuna vingine watu wakisoma kwa kutumia ebook tu basi inatosha. Sasa ukiwa unajua soko lako ni lipi hii itakusaidia kijua ni wapi uuze vitabu vyako na kwa njia ipi zaidi.
8. Format
Jinsi ya kuformat manuscript yako unaweza kutumia word processor yeyote ile uliyonayo. Baada ya hili ni lazima ukiweke kitabu chako katika PDF format. Sehemu za kuchapisha wanapendelea format hii ila bado kuna wengine wanakubali kwa njia ya posta
9. Printing
Kama unatumia e-readers kama (Kindle) kuchapisha kitabu haihitajiki lakini kama unaviuza hard copies (paperback cover etc) ndio unatakiwa kujua hili. Mimi natumia (POD) Publishing On Demand ni ghali kidogo kuliko kama ningeprint vitabu 10,000 kwa mara moja. Hii inanisaidia vitabu vyangu viwe vinakua printed tu pale kikiwa kimenunuliwa.
10. Good luck
Hii utahitaji sana kwa sababu kama huna uvumilivu kuna mambo mengi sana yanaweza kukukatisha tamaa. Mimi kitabu cha kwanza nilikua nafikiria naelewa lakini nilipata shida sana na pia kitabu cha tatu ambacho kilikua ni kitabu cha kwanza kuwa na picha za rangi kilinipa nacho shida sana.
Note: i) Kama unataka kuandika kitabu na kuwapa watu unaowafahamu basi ISBN sio lazima kununua.
ii) Kama hutatumia self publishing companies basi jaribu kutumia Guru.com and thumbtack.com huko ndio mimi napata vibarua (freelancers) wakufanya kazi kwa bei rahisi. Ila kuna thumbtack.com ni ghali kidogo.
Natumaini haya maelekezo nimekaa nikaandika kwa urefu yatawasaidia wale wote wanaotaka kuandika na kuchapisha vitabu vyao. It is not easy but once you finish the accomplishment and holding a book in your hands with your name on it that feeling is priceless.