Thursday, February 05, 2015

Jinsi ya Kuchapisha Kitabu Peke Yako (Self Publishing) Part 1

Baadhi ya watu wameniomba niandike jinsi ya mtu atakavyoweza kuchapicha kitabu peke yake (Self Publishing). Zipo njia nyingi lakini hivi ndio jinsi nilivyoweza kuchapisha vitabu vyangu vyote mpaka sasa hivi. 

Mpaka sasa hivi ninavyoandika hii post nimeshachapisha vitabu vitatu (3) (Modern Swahili, Swahili For Teens My First Book of Swahili Words) na vingine vinne (4) ambavyo ni (Kids in the Swahili Mom Kitchen, #SwahiliMom Kitchen, East Africa Cook Book Jifunze Kiingereza) vinakuja hivi karibuni kwa kutumia njia hii hii. 


Kabla sijaendela zaidi nataka ufahamu haya:-
1. Kama unataka kuandika kitabu ukifikiria utapata hela ya haraka haraka au kuwa tajiri overnight ni heri ukaacha kuendelea kusoma maelekezo yangu kwasababu utakua unapoteza muda wako tu. Kwangu mimi writing and now publishing is just a hobby. Nimeshaandika vitabu vingi sana ila sikufikiria kabisa kama kuna siku ningeweza kuchapisha hata kitabu changu kimoja. Nikiwa mdogo nakumbuka baba yangu (RIP) aliandika kitabu na alihangaika sana kutafuta publisher na hakufanikiwa kupata wa kuchapisha. Thanks God sasa hivi self publishing imeweza kurahisisha mambo na kuondoa ukiritimba uliopo katika hii industry. 

2. Kuchapisha kitabu itakugharimu hela sio free. Gharama hizo ni lazima uweke budget ya $300 - $3000 kwa kitabu kimoja. Hizi gharama zinatofautiana kutokana na mahitaji ya mtu na mtu  Pia usisahau gharama za kukitangaza kitabu chako. Ni kazi ngumu lakini kama unapenda the reward is priceless. Mimi huwa natumia Guru.com kutafuta vibarua wa kufanya mambo mbalimbali na ndio rahisi kuliko ningeingia kwenye contract na self publishing company yeyote ambazo niliresearch na kuwasiliana nao na wakanipa gharama zao. 

3. Kama nilivyosema hapo juu kuna self publishing companies nyingi tu, hivyo kama unataka kurahisisha kazi zako ni bora kuresearch na kuona ni yupi atakua mzuri kutokana na mahitaji yako. Ila hakikisha unaelewa contract unayosign.

4. Hakikisha unaandika topics unazozipenda au unazozijua. Kama hutaenjoy kuandika acha kupoteza muda wako kwavile final product haitakua nzuri. Na pia ikiwa unaandika na hupendi unachofanya hata kama hutapata hela lakini unakua umefurahia rohoni na ukiweza kurudisha hela uliyotumia kutengeneza kitabu chako au zaidi inaongeza furaha yako mara dufu. 

inaendelea........