Tuesday, January 02, 2024

Top Best User-Rated Tanzania Survey Sites 2024

TGM Panel

Score 82.58%


American Consumer Opinion

Score 62.26%


MOBROG

Score 58.42%


SurveyTime

Score 53.33%


SurveySavvy

Score 51.00%


Ipsos i-Say

Score 46.07%


OpinionWorld

Score 39.08%


QuickThoughts

Score 32.97%


Univox Community

Score 26.16%


Hitpredictor

Score 65.26%


Thursday, November 23, 2023

Welcome to Dar Es Salaam, Tanzania 2023

These are pictures of different places in Dar Es Salaam City in Tanzania. It's a husling and bustling city but I'm positive sure you'll enjoy your stay. 

Just don't say "Jambo" as every time you say that as a greeting and you're about to buy something, the price of whatever you're about to buy will miraculously go up.

Locals or someone who knows or have been to Tanzania before don’t say Jambo. They say Mambo. 

Thank me later.  πŸ˜ƒ

Monday, August 16, 2021

Jinsi ya Kujipatia Kipato kwa Kutumia Survey Tanzania

Watu wengi wapo nyumbani kwa vile hawana ajira. Je unajua unaweza kutengeneza hela kwa kufanya utafiti kwenye mitandao?

Kuna sites ambazo ukifanya utafiti au kuangalia video clip au viral videos wanakulipa. 

Cha kufanya  ni  kupakua app au kuingia kwa tovuti ya kufanya utafiti huo na kujisajili. Ukishajiunga utatumiwa barua pepe na maelekezo  mengine ya jinsi ya kufanya ili uweze kulipwa. 

Baada ya hapo ukiwa tayari unaingia kwa app au tovuti uliyojiunga na kuanza kujaza tatafiti yako au kuangalia video clip. 

Hakikisha ni  sites halali za  kufanya  tafiti hizo. Hazihitaji mtu kulipa hela  yeyote ili kujiunga. Ni bure kabisa. Ukiona umeingia kwa  site na wanataka uwalipe  hela  kujiunga, kimbia. Hiyo  itakuwa  ni site  ya  utapeli.

Baadhi  ya site  halali ni hizi:-

Ipsos I-Say. Zinalipa kuanzia $15.

Pinecone Research. Zinalipa kuanzia $1.

    Toluna. Zinalipa kuanzia $5.

    Inbox Dollars. Zinalipa kuanzia $30.

    My Survey. Zinalipa kuanzia $10.

    Swagbucks. Zinalipa kuanzia $5.

    Point Club. Zinalipa kuanzia $10.

    Nielsen Digital Voice. Zinalipa kuanzia $50.

Monday, May 03, 2021

CHAKULA CHA NYUMBANI (AFRICA YA MASHARIKI)

Chakula cha nyumbani ni kitabu nimekuwa nikikiandika kwa muda sasa. Kama ilivyo jina lake kitabu hiki kinahusu vyakula mbalimbali vinavyotokea katika eneo la Africa Mashariki. 

Kama una chakula chako unachokifahamu na ungeoenda watu wengine wakifahamu pia, nitumie jina la chakula hicho ili nikiweke katika kitabu changu. Nitaweka jina lako kuwa wewe ndio umetuelezea kuhusu chakula hicho. Mimi nitajitahidi kufanya uchunguzi na mambo mengine kuhusu chakula hicho na nitajifunza jinsi ya kukipika pia ili niweze kuelezea watu jinsi ya kukipika. 

Vyakula hivi hata kama originality yake sio Africa ya mashariki ila sasa hivi kimezoeleka sana na kuwa kama mwanzo wake ni maeneo hayo wewe nitumie tu. 

Kutafakari (Meditation)

Mimi sio mwanasaikologia hivyo sitaandika kama mmoja wao ila nitaandika kuhusu meditations kutokana uchunguzi niliofanya na uzoefu nilionao.

Nilianza kufahamu kuhusu meditations kama miaka 15 hivi iliiyopita. Nilitambulishwa na boss wangu mmoja ambaye alikuwa ni mwenye asili ya kihindi. Alikuwa yeye anaweza kutulia katika situation yeyote. Hata jambo liwe ni la aina gani yeye alikuwa anabakia kuwa mtulivu sana. Ndio siku moja katika kuongea akaniambia yeye anafanya meditation kila siku asubuhi na wakati mwingine hufanya asubuhi na usiku. Wakati huo kulikuwa hakuna information nyingi kama ilivyo sasa hivi hivyo alinipa kitabu.  

Nilikisoma kitabu hicho na kuanza kufanya pole pole ila yeye alichoniambia au alivyokuwa anafanya ni kukaa na kuwasha mshumaa na kuangalia ule mshumaa kwa makini bila kufikiria kitu kingine (focus). Hivyo nilikuwa nafanya wakati wa usiku na kuzima taa na kuangalia huo mshumaa tu. Aliniambia nianze kwa dakika moja na baada ya muda niendelee kuongeza muda. Nilikuwa nafanya kwa muda wa dakika tatu au tano tu.

Nilifanya hivyo ila nilijikuta nasahau kufanya siku zingine. Yaani kwa ufupi sikuiweka meditation kama sehemu ya ratiba ya kila siku. Ila nilipokuwa  mjamzito kama mama kwa mara ya kwanza kuna programs nyingi mtu akipenda anajiandikisha. Hivyo mimi nilijiandikisha na kwenda kufanya yoga ila tukaanza kufundishwa umuhimu kufanya meditations tena. Hivyo kila siku pamoja na mazoezi mengine ila nikawa nafanya meditations. Mimi ni mtu muoga sana na nina wasiwasi sana ila hakuna kipindi katika maisha yangu niliweza  kuwa mtulivu kama kipindi hicho. Kila nikienda kwa clinic nilikuwa nipo sawasawa kabisa nikipimwa blood pressure ilikuwa ipo sawa. 

Hivyo nilifanya meditations kila siku katika kipindi chote nilichokuwa mjamzito na pia mwaka na nusu hivi baada ya kujifungua.Ila kwa vile nilikuwa sijaelewa umuhimu wa meditation au sikuappreciate nikajikuta naanza taratibu kusahau tena kufanya. 

Sasa covid ilipoanza na lockdown ikachangia watu wengi sana hapa kuanza kuwa na depression au anxiety. Kanisani mchungaji akawa anazungumzia sana jinsi watu wanavyomweleza wanavyosumbuluwa na depression na anxiety. Na mimi wakati wa winter nikajikuta kitu kidogo tu kinanipa wasiwasi. Habari za misiba inayosababishwa na covid nchini Tanzania nayo ikaniongezea wasiwasi sana. Hivyo nikaanza kuona katika kila mkutano ninaoshiriki  tunaanza au kumaliza kwa kufanya meditation. Kanisani wakaleta mtu akafundisha "Christian meditation". Siwezi kusema kuwa niliona tofauti zaidi ya kutumia maneno yaliopo katika bible wakati wa kufanya meditation.

Hivyo nikajikuta narudi kufanya meditation tena. Na kitu ninachokiona ni kuwa nimebadilika na kuwa calm kwa mapema sana. Nimejikuta naweza kuchambua au kuchukua muda wa kupumua kabla sijafikia kwenye uamuzi ya kitu fulani. Wasiwasi niliokuwa nao ukapungua sana. 

Kwa vile sasa hivi kuna maelezo mengi sana online kuhusu meditations ikawa ni rahisi sana kwangu kujua tofauti za meditations na njia ya kufanya meditation. Hivyo ikanisaidia sana kuona mafanikio mapema zaidi. 

Thursday, November 05, 2020

Jipende- Urembo wa Asili

Jipende - Urembo wa Asili by Pauline  Mandari 

Jipatie copy yako bure kabisa kutoka katika channel ya Jipende inayopatikana katika App ya Telegram 

Jipende - Urembo wa Asili

Kwa muda mfupi pakua copy yako bure kabisa ya kitabu cha Jipende - Urembo wa Asili kutoka kwa Telegram App. Tafuta channel ya Jipende au fungua hii link hapa Jipende

Tuesday, November 12, 2019

πŸ’•DIY Oatmeal Bath Powder.πŸ’•

This #oatmeal bath powder is a must for winter. My daughter has a very dry skin. Sometimes I use the #Aveeno oatmeal soothing bath treatment but I love to make it at home as it's cheaper and I know exactly what has gone into it.. 🍯
.
It is super easy to make and I always make more to use for up for a month.

Ingredients 
2 cups oats
1/2 cup baking soda
1/2 cup brown sugar
1/4 cup coconut milk powder or dry coconut flakes. 

Directions
Mix everything in a blender or a food processor. I prefer my #nutribulletrx as it makes a more finer powder than the food processor.

Store in a tight container in a cool dry place. 🎁 It makes a good gift too.

How to use it..... Run bath water and sprinkle 1/4 cup of oatmeal bath mixture. Soak in the oatmeal bath for 20 mins or more if desire. 

🍁Note.🍁
If I don't have the coconut powder of dry coconut flakes,, I use the organic milk to make a paste. Rub all over and the body and wait for 10/15 minutes. Rinse with clean water. .
I use on my daughter during the winter time every weekend and keeps her out of itchy skin for the whole winter. Prior to that starting using this we were prescribed so many different skin creams or use the over the counter Cortisone. Never again for over 7 years now.

For me I use it once every two weeks and helps to keep my skin hydrated really really well.

ENJOY!πŸ’ƒ

Tuesday, October 01, 2019

Jinsi ya Kutengeneza Serum ya Kutunza Ngozi ya Uso

Serum ni kitu muhimu sana kutumia katika utaratibu wako wa kila siku wa kutunza ngozi yako ya usoni. Hii ni moja ya aina za serum ambazo ninazitumia. Hakikisha hutengenezi nyingi sana kwa mara moja kwa sababu huhitaji kutumia nyingi sana kila siku unapotumia, hivyo kiasi utakachotengeneza inaweza kuwa nyingi sana na kukaa hata mwaka mmoja. Ili iwe na ubora mzuri ni muhimu kutumia kwa miezi sita na siyo zaidi toka ulipoitengeneza. Weka kwenye fridge ambayo huhitaji kutumia kila siku mpaka wakati unapoihitaji. 

Kitu kingine cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa unatumia mafuta ambayo ni bora. Ubora wa mafuta yako unayotumia ndio utakusaidia kufanikisha kupata matokeo mazuri unayohitaji kufikia. 

Hii serum ni ya kupunguza ngozi yako kutokua haraka. (kupigana na uzee). Unatakiwa kutumia mara mbili kwa siku baada ya kuosha uso wako na kutumia toner kama unatumia au kama hutumii toner basi ni kabla ya kupaka moisturizer yako unayotumia kila siku.

Thursday, November 30, 2017

Kwa wale walioniandikia kuwa wanahitaji kununua vitabu vyangu vya Kujifunza Kuongea Kiingereza lakini wanashindwa kuvinunua online kuanzia tarehe Dec 1st 2017 mpaka Dec 31st 2017 kwa anayehitaji kimoja au viwili waniandikie kwa Facebook au kwa Twitter au kwa publisher kwanzapress@gmail.com watapata number ya simu ya kutuma hela zao. 

Hela ya kutuma ni gharama ya kununua vitabu tu, gharama ya kutuma vitabu hivyo kufika TZ usiweke.Vitabu vitaletwa bila gharama yeyote. Tafadhali zingatia muda kwa sababu sasa hivi havitakuja vitabu vya ziada. Wale watakaotuma hela zao kwa muda huo ndio watapokea vitabu vyao January 2018. 

Ukianianikia utapewa maelekeo yote yatakayowezesha niweze kuhakikisha kila kitu kinakwenda kama kinavyostahili. 

Shukrani