Je ni watanzania wangapi wanajua katiba ya nchi? Ni watanzania wangapi wanajali kuijua katiba ya nchi? Watu wengi hawapendi kuijua katiba ya nchi kwa vile hawajali. Je usipojali katika kujua sheria za nchi yako nani wa kulaumiwa?
Kila siku tunaona mambo ambayo mengine ni ya kuhuzunisha kabisa, mengine ni ya kusikitisha na mengine ya kuaibisha yanafanyika Tanzania lakini tunajua haya yote ni kwa nini yanatokea? 99% ni kwa vile watu hawajui sheria za nchi na viongozi waliochaguliwa wanapoona hakuna anayejali basi wanafanya vile wanavyopenda. Mwisho wa yote mambo mengine yanapotokea ndio watu wanakufa, watu wanalalamika na serikali inazidi kupoteza imani kwa wananchi wake. Kumbe ni mambo madogo madogo ambayo kila mwananchi angeyajua basi yangeweza kuwafanya viongozi waliochaguliwa kuwa makini katika kila jambo wanalolifanya kwa vile wanafahamu kuwa wananchi wanaelewa.
Mwananchi yeyote uwe umezaliwa kwenye nchi ambayo unayoishi au wewe ni wa kuhamia lakini ufahamu wa kujua sheria za nchi ni wajibu wako. Unapojua sheria za nchi haitakua rahisi kuzivunja. Kuna wengi wanavunja sheria lakini sio kwa makusudi ni kwa sababu hawazijui sheria za nchi zinasemaje. Na pia ukijua sheria ya nchi yako utajua zipi ni haki zako kama raia na ukionewa au mtu akitaka kukushutumu basi utajua kipi cha kufanya.
Changamoto kwa kila mwananchi ni kuijua katiba ya nchi ili kuweza kukusaidia kujua haki zao. Usisubiri mtu akusomee kitabu tafuta kitabu usome mwenyewe. Ukisomewa mwenye kusoma anaweza kuruka ukurasa au kutafsiri apendavyo. Mambo ya kukaa chini kusomea vitabu umepitwa na wakati. Ni wajibu wako kujua haki zao...
Tusikalie kulalamika tu mara baada ya kitu kufanyika ni wajibu wako kama raia kuuliza mfanyakazi wako ni kwa nini kitu fulani kinafanyika hivi njea ya katiba ya nchi. Kuwa na moyo wa kuijua katiba ya nchi na kujua hakizako, kuwa na moyo wa kupenda kufuatilia yaliyosemwa na viongozi ni nji moja wapo itakuondoa katika mambo mengi sana yanayotokea nchini. Kama tunavyojua viongozi wengi huwa wanasema tu kile wanachotaka wananchi kusikia kwa vile wanajua hakuna atakayefuatilia.
Watu wengi hawaelewi nchi ni kampuni na mwananchi ni investor. Unapochagua kiongozi huyo kiongozi anafanya kazi kwako. Sasa ni wajibu wako kupenda kuuliza maswahi ukiona mahesabu hayabalance. Ukiinvest hela kwenye kampuni yeyote kila siku unafuatilia ili uone hela yako uliyoweka huko inaendeleaje. Sasa kwa nini unaivest maisha yako kwenye nchi na wala hupendi kufuatilia kujua ni nini kinaendelea kutokea ngazi za mitaa hadi za juu za taifa.
Ni wangapi mikutano ya mitaa ikitokea wanakwepa kwenda? Ni wajibu wetu kama tunataka hizi ajali zipungue tuanze kuwajibika na kushiriki katika mambo mabali mabali. Kama tunataka rushwa ziishe ni wajibu wetu kuhakikisha unajua haki yako.