Friday, September 23, 2011

Jinsi ya kutafuta michango ili kusaidia kuendeleza blog yako

Nimepokea maswali mengi ya bloggers wakitaka kijua jinsi ya kuweza kuingiza hela ili ziwasaidie kuweza kutunza blogs zao kama hawana wafadhili. Hivyo nimeona kuliko kujibu mtu mmoja mmoja basi nimeona nipost hapa ili mwenye kutaka kufanya hivyo asome yote na kuangalia ni njia gani itakua rahisi kwa yeye kufikia malengo yake. 

a. Ni kuweka donation button kwenye blog yako. Hiyo itawafanya wasomaji wa blog yako wanaopenda kukusaidia watatumia hiyo njia kukutumia hela. Donation button unaweza fanya kwa kutumia paypal. Tafadhali soma hayo maelekezo ya kuweka donation button hapo ameelezea vizuri sana..

b. Ni kuweka baadhi ya post zako kuwa za kulipia na sehemu zingine ziwe za free. Hiyo unaweza kufanya kwa kutumia mailchimp service ambayo basic service yake ni bure. Ila wao wanahitaji uwe na Amazon associates ID ili uweze kupokea hela zako. Na Amazon associates ID unaweza kuipata hapo na sio lazima uwe unaishi USA

Tafadhali ukumbuke kila kitu kinahitaji juhudi nyingi. Hivyo si kuwa ukishakua na hizi njia basi ndio hela zitaingia haraka na kirahisi. Ni kutokana na yale unayopost kwenye blog yako na jitihada zako unavyojitangaza ili watu waifahamu blog yako zaidi.

Good luck