Tuesday, March 25, 2014

Tafuta Partner na sio Mfadhili



Inafurahisha sana kuona jinsi vijana wangi sasa hivi Tanzania wamegundua kuwa na college degree sio solution ya kupata ajira. Wamegundua kuwa kuna njia nyingine ya kuitumia elimu yao kwa faida yao na jamii kwa ujumla. Njia kuu moja wapo wamegundua kuwa ni wao kutengeneza ajira ili kuendeleza maisha yao na kuwapatia watu wengine ajira. 


Inafurahisha jinsi vijana wengi Tanzania walivyo na visions, ideas nzuri na hata wengine pia wameshafikia kuanzisha biashara zao tayari na kinachowakwamisha ni kukua kwa biashara zao kwa ajili ya mtaji ni mdogo walionao.


Nimekua nikipokea direct mails kwenye Twitter au emails nyingi tu za vijana Tanzania wakinielezea mambo yao mazuri sana tu wanayoyafanya lakini wengi wao huwa wanataka mimi niwasaidie kutafuta “SPONSOR”. Sasa kila email au DM inayokuja inaeleza mambo mazuri sana lakini mwisho wa yote ni kuwa mtu anataka sponsor. Sasa mimi nimekua nikijiuliza sponsor ni just a new trendy au ni njia nyingine ya mtu kushindwa kujua ni vipi atapata capital ya biashara yake?


Nimeona niandike hapa ili kila mtu mwenye mawazo hayo aelewe. Naweza niwe wrong lakini haya ni mawazo yangu na nafikiri kidogo ndio ulimwengu wa leo unavyokwenda.

  1. Always katika biashara hakikisha wewe ndio the big risk taker bila hivyo hiyo biashara haitafanikiwa. Katika hili naona kuwa vijana wengi Tanzania sio risk takers. Mimi nafikiria kwanini wengi wanatafuta sponsor tu badala ya kufikiria njia nyingine ya kuraise capital. Mimi naona ni kwavile hawataki kutake risk. Kama biashara anayoifikiria ikifa basi yeye anakua hana hasara bali hasara inakwenda kwa yule “sponsor”.  Ulimwengu huu hakuna mtu atakayekuamini nakukupa hela yake kwa vile umemueleza ideas na visions zako nzuri sana.
  2. Usipende kutajirika mwenyewe kama unahitaji mtaji na una idea ya jambo zuri sana basi tafuta partners unaowaamini na wao waweze kukuamini. Kila mtu akija na kiasi fulani cha hela basi mnaweza kuanza kazi yenu na mkishakua na cha kuonyesha basi mnaweza kwenda kwa watu wengine zaidi na kuwajumuisha na kukuza capital zaidi ya kazi yenu. 
  3. Hakikisha kabla hujaanza kutafuta partners au hata kama ni kuomba mkopo bank umeshafanya research kuhusu hilo jambo unalotaka kuanzisha. Wengi nikiwauliza umeshafanya research na kuona kuwa kuna market ya hicho kitu? Jibu ninalopata ni kuwa anatafuat kwanza mtaji halafu akishajua amepata ndio anakwenda kufanya research . Anafikira kupoteza muda mwingi kufanya research halafu asipofanikiwa kupata hela basi inakua ni kazi kubwa isiyo na faida na muda unakua umepotea bure. Sasa ukweli ni kuwa hakuna mtu atakupa hela yake bila kujua kuwa uachotaka kufanya kitarudisha hela yake na hata faida pia. Kama ni startup yeyote fanya kwanza research ujue kuwa kuna market, na kama sio startup basi angalia je mtu mwingine anafanya hicho unachotaka kuanzisha soko lake ni kubwa kiasi gani? Kama soko lake linakidhi mahitaji ya watu je wewe ukianzisha utapata wateja kutoka wapi? Je wewe utafanya nini zaidi ili kuwafaya wateja wake waache kwenda kwake na kuja kwako? Je growth ya hicho kitu ni kipi etc. Hayo yote unatakiwa kuyajua kabla ya kuanza kutafuta capital au kuwekeza hela nyingi.
  4. Kama unataka kupata hela kutoka bank ni lazima uandike business plan. Business plan ni nzuri kwa bank au hata kwa watu binafsi kuweza kuelewa dira yako ni ipi na kukuamini hata wakiweka hela yao wanajua wataipata na kupata faida.Pia business plan ni nzuri kwako kwa vile inakuonyesha ni wapi unataka kwenda na kukua kwako kutatokana na nini?
  5. Kumbuka hakuna mtu yeyote hata kama ana hela kiasi gani hataki kupata faida katika hela yake. Sasa ili kufanikiwa katika kupata au kuongeza mtaji wa jambo lolote unalotaka kufanya ni lazima uwe umeonyesha kuwa unalolifanya unalielewa, unaliamini  na wewe umewekeza kiasi kikubwa ambacho kitakufanya uwe na uchungu na kufanya kazi kwa bidii na umakini.
  6. Uza share za biashara yako. Kama umeshaona kuwa unachokifanya kina mafanikio basi uza share ili uongeze mtaji. Unaweza kuwauzia ndugu na rafiki zako na kuongeza mtaji kabla hujaanza kutafuta watu ambao hawakufahamu. Hiyo ni njia mojawapo ya kukusanya capital.
  7. Nenda bank kachukue mkopo. Kama kweli unachotaka kukifanya unakiamini kuwa kitarudisha hela ya watu na kukupatia faida basi andika business plan uende bank ukachukue mkopo. 

Sitaki kuingia siasa hapa lakini nafikiria kuwa misaada mingi haifanyi kazi Tanzania kwa sababu watu hawana uchungu na hiyo hela, hawajui waliowachangia wamejinyima kiasi gani ili kuweza kuwapatia hiyo hela na pia wengine wanafikira huko kwa wafadhili money grows on trees. Wanajua jambo wanalofanya lisipofanikiwa kesho watalia tena na atatokea mfadhili mwingine na kusaidia lakini je hujali muda unaoupoteza?  Huoni kuwa unazeeka bila maendeleo yeyote.
Katika jambo lolote unalotaka kufanya ili ufanikiwe hakikisha umewekeza sana either pride, muda wako, hisia zako au hata kiasi fulani cha hela kabla hujanza kutafuta watu. Bila hiyo chochote unachotaka kufanya hata ukipewa hela kiasi gani hakifanikiwa. Jiulize niw watu wangapi kila siku wanaomba mitaji na biashara zao zinakufa, kesho tena wanaenda kwingine kuomba mtaji tena? Ni kwa vile mtu hajafanya research ya kitu anachokifanya, hajakaa chini na kuangali growth ya hiyo biashara itatokea wapi? Je kukua kwa hicho kitu kutatokana na nini? Angalia watu wengi wenye biashara nzuri, zina faida kubwa lakini hata baada ya miaka 10 yupo pale pale au mwisho wa yote wanatokea watu wengine na kufungua bishara kama yake na kuchukua wateja wake na kufanya biashara yake ipungue, ibakie kama ilivyo au inakufa? Sababu mojawapo ni kuwa hakuwa na growth plan or exit strategy.  Unaweza kuwa na idea nzuri na biashara nzuri lakini unforeseen future changes (ndoa, familia, maradhi etc) katika maisha yako zikakufanya usiweze kuwajibika katika shughuli yako 110%. Sasa exit plan ni ipi?

Natumaini maelezo yangu yatakusaidia ili usije kukata tamaa ya idea yako nzuri. Idea inaweza kuwa nzuri lakini kila unayemwandikia kumwomba ufadhili au akutafutie wafadhili hawakusikilizi kwasababu katika biashara hakuna cha ufadhili. Business ni business. Hakuna charity katika business. Ukiwa kwenye business au ukiwa unataka kufanya biashara ongea lugha ya business.