Friday, February 28, 2014

Nitakachoweza na Ambacho Sitaweza

Ukiona kila siku na tweet sio kua sina jambo bora zaidi la kufanya ila natumaini sauti yangu au sauti za wengi katika mambo mbalimbali zitasaidia kubadilisha muundo wa wa utendaji wa serikali ya Tanzania, uwazi, uwajibikaji, utunzaji wa hela au kuwajibika katika kuona umuhimu wa kuboresha huduma za jamii ili maisha ya watanzania wengi wanaotegemea huduma hizi au ya watu wote yaweze kuboreshwa. Au kuweza kusaidia kuweka system, policies au justice system ambazo zitaweza kusaidia yule mtu atakayeweza kujishughulisha kwa bidii aweze kufanikiwa. 

Hizi emails na message ninazozipata kila baada ya siku moja ua mbili huwa zinaniumiza roho sana. Huwa najiuliza ni kila mtu anayeishi nje ya nchi anapata hizi emails, watu hupenda kuniambia vitu vyao vya binafsi kwa kuniamini, kwasababu mimi ni mwepesi kuongea na watu na ni msikilizaji wa mzuti au kwasababu mimi ni mwanamke & mama. lAll in all huwa na appreciate mtu akinavyofikia kuniamini na kuniambia vitu vyake vya binafsi but vingine vipo too big & too much for me to handle. Na kama binadamu roho huwa inaniuma nikishindwa kumsaidia mtu.  Ingawaje baba yangu (RIP) alikua ananiambia wengine hawana shida wanazokuambia wanakutapeli tu wakiona unaishi huko wanafikiria hela mnazo nyingi sana au zinapatikama kirahisi.

Anyway jambo ninalotaka kuweka hapa leo ni hili ili kabla hujaniandikia ujue nini nitaweza kukusaidia na nini sitaweza kukusaidia. Kwanza elewa kuwa kua mimi ni mtu wa kawaida mwenye majukumu ya maisha kama watu wengine. Sina a lot of disposal income kama watu wanavyofikiria. Na pia labda nipo content kwasababu watu wengine wanaoniomba misaada wana uwezo mkubwa kimaisha kuliko mimi. Huwa napenda kusaidia watu lakini ni pale kadri ya uwezo wangu. na pale ninapoweza. 


Please soma uangalie kama naweza kukusaidia au la. 

Nitakachoweza kukusaidia
1. Ushauri katika biashara kama umeshaanzisha au unamtaji lakini hujajua nini unataka kuanzisha.


2. Ushauri katika career path yako kama upo karibu kumaliza shule high school au college au umeshamaliza shule.


3. Ushauri katika masomo yako kama bado hujachagua major au umeshachagua major lakini bado unahitaji some guidances.


4. Ebooks kama kitabu unachotafuta kipo katika public library yangu naweza nikakiazima nikakutumia.


5. Kama unahitaji kitabu hard copy format lakini hakipatikani Tanzania naweza kukiangalia kama kinapatikana kwa bei gani na ni juu yako kulipa gharama zote za kitabu na postage.

6. Any information kama ninafahamu nitaweza kukusaidia according to the knowledge I have.


7. Siku hizi kila kitu kinapatikana online kama ukigoogle sio kama zamani hivyo natumaini information za college mbalimbali zipo online lakini kma unahitaji ushauri au jinsi ya kuapply nawea kukusaidia lakini application fee zote ni juu yako. 

Mambo ambayo sitaweza kukusaidia


1. Kama una jambo lako na unaona kuniandikia haitawezekana hivyo ni lazima uongee na mimi basi ni wewe unipigie simu. Siwezi kukupigia simu wewe ukiwa Tanzania. Na pia kama nimekupa number yangu ya simu sio kuigawa tu kwa watu wengine bila idhini yangu. Pia kuna tofauti ya masaa hivyo zingatia hilo ukinipigia simu usiku wa manane nakublock na sitahangaika hata kusikiliza tatizo lako. 

2. Siwezi kukusaidia msaada wowote wa kifedha either ni hela ya mtaji wa biashara au kujikimu kimaisha wewe na familia yako au ukiwa upo chuoni.

3. Laptop, simu za mkononi, brand name clothes, sandals, handbags, perfumes, sunglasses bei zake ni za juu tu kama ilivyo Tanzania. Tofauti ya huku na Tanzania ni kuwa huku ukienda kwenye maduka halali hutauziwa refurbish, fake au knockout. Na pia ukiona kitu ukumbuke huku vitu wanaweka bei kabla ya kucharge tax. Hivyo kitu chochote bei yake ni hiyo unayoiona + 6% to 7.5% tax inategemea kipo state gani. 

4. Siwezi kukusaidia kutafuta sponsor/partner wa biashara yako yoyote au kukusaidia kufund idea au project yako yeyote. Sijui wafadhili wowote ambao wataweza kukusaidia kwa hilo. 

5. Siwezi kukuconnect kwa Mr Mengi. Yupo hapo kwa twitter. Unahitaji anything kwake kama mtaji au kazi please tweet to him natumaini atakusikiliza.


6. Siwezi kukuandikia barua ya sponsor ili uje kutembea au kutafuta maisha huku niliko. Kwanza siku hizi kwa wale wanaotaka kuja kutembea tu ni rahisi kupata visa kuliko wale wanaotaka kuja kusoma. Sasa kama unataka kweli kuja tu kutembea na una hela ya kufanya hivyo ukienda kuomba visa watakupa kirahisi sana. 

7. Siwezi kukupa financial statement yangu ili uweze kupata visa uje kwenye shule uliyopata tayari huku. Shule ziko nyingi na kupatikana ni kwa urahisi sana tatizo ni financial support kama huna scholarship. Sasa please ukiwa unatafuta shule ujue na jinsi utakavyopata financial statement ya kuonyesha kwamba utaweza soma bila matatizo. Usije ukapoteza hela za application fees wakati hujajua utapata wapi hiyo barua. 

8. Siwezi kukupokea au kupokea mtoto wako akiwa anakuja huku kusoma au kuanza maisha. Kama ni kukusaidia kukaa kwangu sio zaidi ya week moja na inategemea na muda au uwepo wa nafasi hiyo. 

9. Siwezi kuja kukupokea airport au kumpokea mtoto wako airport. 

10. Siwezi kukupa ushauri wa matibabu yako au ya familia yako. Kama nikikupa ni jinsi ya ufahamu wangu wa ugonjywa huo na sio kuwa mimi ni mtaalamu. Ushauri au maelezo yangu ni kutokana na jinsi ninavyoelewa na isiwe ndio ushauri wa mwisho. 

11. Siwezi kukutafutia mchumba. Mimi ni wa mwisho katika familia yetu na my big sisters wote wameolewa hivyo sina mdogo ambaye naweza kukuhook naye. 

12. Siwezi kukupa ushauri kuhusu mume/mke wako kwanza kama hatujawahi kuonana, siwezi kabisa na sipendi kabisa kufanya hivyo kwasababu I tell like it is. Sasa usije ukaniambia kitu kuhusu relashionship yako nikaja nikaongea kitu kesho outcomes za maongezi yetu yawe usivyopenda uje unilaumu mimi. Kama jambo lako la ndoa yako onana na watu wakuu wa dini yako. 

13. Mwisho ni hizi never endings michango za Tanzania. Mimi nimeweka budget yangu kwa mwaka ambayo inacover sadaka for my personal faith & donation (half goes here where I live & half kusaidia where I came from -Tanzania) na kwa Tanzania niliona hilo fungu lake ni heri niwe nasaidia kwa kusomesha wanafunzi. Hivyo ninaowasomesha nao wakimaliza shule na kuanza maisha natumaini na wao pia watajitahidi kusaidia mtu mmoja au zaidi naye aweze kusoma na kumaliza shule. To me that is a gift that keeps on giving. Sasa hii michango ya leo madawati, mara kesho mabati, mara vyoo, ujenzi wa shule au nyumba ya mwalimu nilishachangia sana na kuja kugundua bila kuwa na accountability au wanaochangiwa kushirikishwa katika zoezi hilo la uchangishaji wa hivyo vitu, hawapati uchungu na hivyo kutovitunza vitu ambavyo wengine wanajinyima ili kuweza kuwachangia. Mwisho wa siku inakua kila baada ya mchango huu ni mchango mwingine tena. Mimi nilikuja  kaa na kufikiria kama watu hawatajifunza kutunza vilivyopo hata vikichangwa kiasi gani havitadumu. Watu kuheshimu mali za umma na utunzaji wake ni tofauti sana na nchi za wenzetu mpaka tutakapoelewa hilo hii michango haina tofauti na kuweka maji kwenye gunia. Mimi niliona bila something to change my money nitasaidia kwingine ninapoona results zinazoniridhisha. 


okay I hope utasoma kwanza kabla ya kunitafuta na kunielezea jambo lako.