Nazi
Maji
Njia ya Kwanza
- Chukuna nazi iliyokomaa sio zile changa.
- Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon.
- Baada ya hapo changanya na maji ya baridi halafu kamua kwa kutumia cheese cloth au chujio kama unalo kuoata tui la nazi.
- Weka katika chupa yenye mdomo mpana na uiweke itulie kwa masaa 24. Au weka kwenye fridge.
- Toa mapovu ya juu. Toa mafuta ya katikati weka kwenye chupa nyingine ambayo ndio utayatumia. maji yanayobakia mwaka chini mwaga.
Uzuri wa kutumia njia ya maji ya baridi ni kuwa mafuta yanakuwa na virutumisho vyake vyote lakini hayakai muda mrefu. Huwa yanaharibika mapema sana.
Njia ya pili
- Chukua nazi iliyokomaa sio zile changa
- Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon.
- Chukua maji ya vuguvugu halafu changanya na nkikono yako kwa dakika moja hivi
- Kamua kwa kutumia chujio la nazi au cheese cloth. Unaweza kurudia mara kadhaa kuweka maji ya vuguvugu ili kutoa mafuta yote
- Ukishapata tui weka katika chupa na kuiweka masaa 24 ili mafuta yajitenge na maji. Au unaweza weka jikoni (medium heat) kwa muda wa saa moja au mpaka maji yameondoka na iliyobakia ni mafuta. Toa mapovu ya juu halafu weka mafuta yako katika chupa utakayotumia.
Njia ya tatu
- Chukua nazi iliyokomaa sio zile changa
- Kuna nazi kwa kutumia njia yeyote uliyonayo kama una mbuzi, food processor, blender, grater au grapefruit spoon.
- Weka nai yako na maji katika jiko (medium heat). Chemsha mpaka uone mafuta yanatokea juu
- Ondoa kwenye sufuria. Tumia kijiko kutoa mafuta na kuweka katika chupa yako
Njia ya nne
- Chukua nazi iliyokomaa
- Iache mpaka iharibike
- Baada ya hapo toa nazi na usiwekek kwenye blendder, food processor ili iweze kulainika
- Chukua maji ya vuguvugu na kukamua tui
- Chemsha tui na mchai chai pamoja mpaka uone mafuta yanabakia
- Ondoa majani na kutoa mafuta yako na kuyaweka kwenye chmbo chako ili utumie
Njia hii inakufanya uweze kupata mafuta mengi zaidi na pia mchai chai unamanufaa sana katika kufanya mwili uwe unarelax sasa ukichanganya wakati wa kuchemsa utaweza kupata virutumisho vyingi zaidi.
Kuweka harufu katika mafuta yako ya nazi
- Chukua safuria kubwa weka maji na kuyaweka kwenye moto. (medi-High).
- Chukua sufuria ndogo weka mafuta yako ya nazi.
- Chukua mchai mchai (green tea. Changanya kwenye mafuta yako.
- Weka safuria ndio juu ya safuria yenye maji na kupika kwa muda wa dakika kama 30 hivi.
- Ondoa majani na weka mafuta yako kwenye chmbo cha kutumia.