Wednesday, June 12, 2013

Maoni Yangu Kuhusu Rasimu ya Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania



First I want to let you know before you read this, you have to know that it took me about a week to put  my  thoughts together on paper so respect my views….And these are just my VIEWS ...that is it....…Nothing more nothing less.......

Now kabla ya kusoma maoni yangu au kusikiliza maoni ya mtu yeyote ningekushauri ujisomee draft hiyo ya katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kwanza wewe mwenyewe. Soma ya zamani na ya sasa hivi ili uone kama kuna tofauti. Soma na kuielewa halafu ndio utajua maoni yako ni yapi, lipi la kuongeza au lipi la kupunguza? Hakuna mtu asiye na maoni katika katiba hii mpya, kama huna maoni yeyote either hujaielewa au huna dira yeyote. 

Pia fahamu kuwa hii ni nafasi ambayo unatakiwa kuitumia kwa makini sana. Kuna watu wengi sana wanazaliwa na kuishi kwa katiba ya nchi waliyoikuta na kufa bila kupata bahati ya kutengeneza katiba ambayo wangependa kuitumia wao wenyewe au watoto wao. Hivyo kwavile umepata nafasi hii ya kuchangia maoni yako katika katiba hii mpya unatakiwa kumshukuru Mungu sana na kuitumia nafasi hii kwa busara sana na pia usiwasahau hao watakaokuja huko mbeleni kuitumia katiba hii. Fikiria kama wewe unavyotumia katiba ambayo mtu mwingine aliiitengeneza inakusaidiaje wewe kama raia wa kawaida? Hivyo unapotoa maoni yako usijifikirie wewe mwenyewe tu bali kumbuka watoto wako, wajuukuu zako na vizazi vinavyokuja ambavyo vitaitumia hii katiba. Huwezi jua katiba nyingine itakuja kutengenezwa lini. So be grateful for having this opportunity and don't take it for granted. 

Okay nikiangalia ni jinsi gani nchi za wenzetu zinaendelea, nimegundua kuwa pamoja na uongozi mzuri na kuwa accountable kwa mambo mengi lakini katiba nzuri, wananchi kujua katiba yao na kuparticipate katika mambo yote ya serikali kuanzia serikali za chini mpaka juu ni jambo moja kubwa sana linalochangia kupata maendeleo hayo. Ninaona kuwa vijana na wazee wengi wanajihusisha katika mambo mengi yanayohusu serikali sana ukilinganisha na Tanzania. Na pia kila kitu chao kinaanzia katika katiba sio Tanzania kila siku mtu anaamka na kutunga sheria zake na kuwaambia watu fanyeni hivi au msifanye hivi bila kujali katiba ya nchi inasemaje? 

Ukija kwenye rasimu hii jambo nililonifurahisha ni kuona jinsi tume hii ilivyojitahidi sana kusikiliza maoni ya watu wengi. Hilo ni jambo la kuwapongeza sana. Miaka ya nyuma ilikua ni viongozi ndio wana sauti ya mmwisho lakini ukiangalia sasa hivi mambo mengi sana niliyokua ninatweet yameingia. Mambo ambayo mimi binafsi nimeona yana mapungufu ni kuwa kama hii tume waliaminiwa na kuteuliwa na kukubalika na jamii kutengeneza katiba mpya basi ni bora wangeweka kila kitu katika katiba hii. Vyote vinavyojulikana vipo sasa hivi au havijaingia sasa hivi Tanzania wangeviweka. Kwavile ulimwengu unabadilika sana na watu wengi wanahamia Tanzania ni lazima miaka ya huko mbele wageni wengi wataleta taibia na mambo ambayo huko kwao ni legal kuyafanya. Ili kwa Tanzania kulinda nchi na kuiweka katika jamii wanayoitaka ni bora kuweka kila kitu Tanzania inavchoamini au kutoamini kikaeleweka. Katiba ndio kioo cha nchi. Katiba ndio inaonyesha nchi imeendeleaje na katiba ndio ya kutunza Tanzania ya mwaka 1961.

Ukisoma rasimu hii utaona kuwa sehemu za mwazoni za katiba ni vitu vingi hawajavigusa kabisa au kuvielezea kabisa wameacha kama katiba ya zamani. Hatujui sababu ya kwanini miaka ya huko nyuma waliacha hivyo au kuachia bunge, dini au jadi na mila kutumia sheria zao, hi swali hatuwezi kulijibu lakini kilichopo sasa hivi ni kutengeneza katiba ambayo itaingiza kila kitu kinacholinda jina la Tanzania na wananchi wake kwa ujumla.  Sasa katiba ya sasa hivi ikiacha mambo mengi bila ya kuyaelezea ina maana inawaachia tena jadi, mila, dini au bunge kutunga sheria hizo.  Nchi ya Tanzania ni ya watanzania na sio ya mila fulani, jadi fulani au dini fulani. na pia tunajua mila na jadi nyingi zina sheira  zinazokandamiza watoto na wanawake. Kuna dini zinazokandamiza wanawake sasa kupata nafasi hii ya kurekebisha mambo hayo na kuacha kufanya hivyo sio kuitendea jema nchi na wananchi kwa ujumla. 

Pia kuacha vipengele fulani na kusema bunge litatunga sheria hiyo sio right pia. Bunge ni wananchi na pia ndio bunge ni la kutunga sheria lakini linafanya hivyo kwavile katiba ikiwa imetengenezwa hivyo vitu  vilikua havipo au vitu vilivyokuwa vimewekwa kwenye katiba vimepitwa na wakati. Lakini sasa hivi wamepewa nafasi ya kutengeneza katiba viwekwe vitu vyote ambavyo viko applicable leo. Huko mbele ikifika wakati bunge linahitajika kubadilisha au kuengeza basi lifanye hivyo. Bunge ni sauti ya wananchi lakini pia wabunge wengi hutetea maslahi yao.
 
Jambo lingine nililoliona ni kuwa kama katiba hii ingetumika kama katiba ya hizi nchi kipeke yake ingekua nzuri na ingekua inahitaji vitu vichache kuongeza au kuvibadilisha lakini kama hii katiba ndio ya muungano basi hizi serikali zitakazotengenezwa zitakua jina tu na hazitakua na mamlaka yeyote. Hii katiba imetengenezwa kwa lugha ya kuonyesha kuwa kutakua na serikali tatu lakini ukisoma zaidi unaona mamlaka yote yapo katika serikali ya muungano. Ukiangalia kwa undani utaona kuwa serikali hizo zitakua na migongano na serikali ya muungano katika utekelezaji wa mambo ya nchi zao kipekee. Katiba hii iwe adopted na kila nchi kipeke yake na kama kila nchi ikitaka kuadd au kupunguza mambo yake basi wafanye hivyo. Halafu warudi watengeneze katiba ya muungano ambayo italink hizi nchi mbili. 

Kwanza kwa katiba hii serikali itakua ni kubwa sana sana. Na kuna ambao watakua hawana kazi ya kufanya lakini wanalipwa tu mishahara especially viongozi wa serikali hizo za chini ya muungano. Na pia bila kusahau siasa, je hebu tufikirie raisi wa muungano akiwa ametokea CHADEMA na wa Tanzania bara awe ametokea CCM kweli kuna jambo la maendeleo  litakalo msaidia mwananchi wa kawaida litafanyika hapo? Ni lazima kufikiria ukweli wa mambo haya kuliko kuwaza kulinda muungano kwanza au kutafuta kutengeneza kaazi ambazo hazitaisaidia Tanzania.  Je faida za kuwa na serikali tatu ambazo zitakua gharama sana kuziongoza zinazidi faida za kuwa na muungano wa serikali?

Kwanza mimi kwa upande wangu ninavyoona sio lazima muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulindwe na chombo kama serikali. Kama huu muungano ndio unaofanya wafikirie kuwa na serikali tatu inabidi wafikirie tena. Ni heri kuwe na chombo kitakacho link hizi nchi na kuweka sheria za kulinda na kunufaisha kwa pande zote mbili. Au kuuvunja muungano hizi nchi zijitengenezee katiba zao peke yao halafu ndio warudi kwenye meza wajadili ni vipi wataweka muungano wao. 

Aumimi nafikria kwa kujaribu kupunguza gharama za kuwa na serikali tatu ni heri wafikirie kuwa na serikali moja na kufanya Tanzania ie nchi ya majimbo. Kuwe na majimbo kama matano upande wa bara na Zanzibar kuwe na majimbo mawili yote hayo yawe chini ya serikali hii ya jamuhuri ya mungano wa Tanzania. hayo majimbo ndio yawe na viongozi wao na katiba zao ambazo zitakua chini ya serikali ya muungano. kwa kufnay hivyo itasaidia sana nchi pia kwa vile kilichokizuri Mwara sio kizuri Bukoba. Kilicho kizuri Tabora sio kizuri Zanzibar. 

Na pia serikali ya majimbo itasaidia kuleta maendeleo katika kila jimbo. Hii ya sasa hivi ya mikoa inayotengeneza hela kusaidia mikoa amabayo haitengenezi hela ianazidisha uzembe. na pia inapunguza ubunifu. kwa wenzetu huku ni kuwa unakuala ulichopanda. Ingawaje central Govt inapeleka hela kwenye majimbo yao kutokana na population ya watu lakini kila mji unamaendeleo kutokana na ubunifu wao na mchango wao katika jamii. Utakuta sehemu zingine zina recreation nyingi nzuri na bure kwa watu wanaoishi hapo lakini sehemu zingine utakuta ni simple tu. 

Na pia sasa hivi hata vijana wengi upande wa Tanzania bara wameshakua na akili ya kujiuliza ni nini faida ya huu muungano? Ni kiasi gani kinatumika kutoka Tanzania Bara kusaidia kuchangia katika maendeleo ya Zanzibar? Na kwa kufanya hivyo je Tanzania  bara wanapata faida ipi? Tunaona upande wa Zanziball ndio wanakua vocal zaidi kutaka huu muungano uishe lakini ukweli hata vijana wengi wa upande wa Tanzania bara wanaanza kuona chokochoko za huko Zanzibar zinaanza kuvuka bahari na kuigia upande wa Tanzania bara. Sasa wanajiuliza hayo yote yanawafikia for the sake of muungano je ni kwa faida gani wanayopata? Hivyo bila kuurekebisha hayo ni kulazimisha huu muungano bila kuangalia gharama za kurun hizo serikali tatu zitagharimu kiasi gani au zitatoka wapi na kuengeza chuki nyingi kwa wale ambao wanachoshwa. Na pia ni kuongeza kurudisha nyuma maendeleo ya nchi kwa pande zote ambayo yanahitajika sana.  

Na pia kwa maoni yangu kama wakiamua kuacha Tanzania ya serikali tatu basi viongozi wa jamuhuri ya muungano wote na wafanyakazi wa serikali ya jamuhuri ya muungano wasiwe wanasiasa au kujihusisha na mambo ya siasa. Wakiachia viongozi hao wawe wanasiasa italeta mgongano kwa nchi ndogo kama Tanzania ambayo demokrasia ya kweli bado ni changa sana. Kwa maelezo ya katiba hii madaraka yote ya nchi ya Tanzania anayo raisi wa muungano lakini utekelezaji wa kila nchi atakua nayo raisi wa nchi pekee ni bora wafikirie hilo mapema. Kama nilivyosema hapo mwanzoni sipati picha iwapo raisi wa muungano anatoka CCM halafu raisi wa Tanzania bara (Tanganyika) anatoka CDM. 

Kama watakua na serikali ya majimbo basi sio vibaya kuwa na viongozi wanasiasa kwa vile kutakua na viongozi wengi katika kila jimbo na huyo raisi atakua anawajibika kwa viongozi wengi wa majmbo ambao kati yao kutakua na wanaotoka katika chama chake na kuna watakao toka kwenye vyama vingine hivyo hawezi kuwa na upendeleo kwa kiongozi au maendeleo ya jimbo moja na kuwakandamiza viongozi wa majimbo membine kwa vile hawatoki katika chama chake. Kuachia viongozi wa jamuhuri ya muungano wawe wanatokea kwenye siasa kutakua na migongano ya ndani na kama ndio hivyo miaka mitano wanayoruhusiwa na uwezekano wa kiongozo kuwa kiongozi kwa terms mbili ni mkubwa sana Tanzania basi inakua miaka kumi isiyo na jambo la manufaa yeyote kwa mwananchi kutokana na viongozi kutokuelewana kwa ajili ya siasa.

Jambo lingine la kubadilisha mimi naona ni kupunguza muda wa kuwa kiongozi kutoka miaka mitano kwenda minne.. Miaka mitano na kuwa unaruhusiwa mara mbili ni mingi sana na inawafanya viongozi wawe wazembe na maendeleo yanachukua miaka 10 tena kubadilika. Just kupunguza mwaka mmoja chini utaleta mabadiliko mengi sana na kutakua na tofauti kubwa sana katika uwajibikaji wa viongozi hawa. 

Kubwa sana ambalo linahitaji kubadilika pia ni kuwa sheria iweke kuwa raisi wa nchi asiwe mwenyekiti wa chama. Hata kama alikua mwenyekiti akichaguliwa tu basi anaachia uongozi wa chama kwa watu wengine. Hii ya sasa hivi raisi ni mwenyekiti wa chama ni mbaya sana. Ukiwa raisi unatakiwa kutumikia wananchi wote bila kujali ni wanachama wa chama gani. Kwanza hata kujihusisha na mambo ya chama iwe mwiko. Ndio sera zake zitakazokua zinatokana na chama chake lakini kujihusisha na chama ni mbaya.

Nimeona pia katika mapato ya serikali ya muungano moja wapo ni ushuru wa bidhaa. Halafu ya pili ni michango itakayotolewa na hizi nchi kwa kuwa member wa muungano huo. Sasa swali langu ni kuwa kama kila nchi itatoa dues zake katika muungano huo hizo ushuru wa bidhaa ni bidhaa gani? Serikali ya muungano itakua na control ya bidhaa za nchi gani iwapo kila nchi itatakiwa kucontrol ushuru wa bidhaa zake ili iweze kutunza serikali zao na kulipa dues za hiyo serikali ya muungano? Na madeni wakikopa ni nchi ipi hiyo italipa lipi au kwa asilimia gani kila nchi itatakiwa kulipa madeni hayo? Kabla hawajafikiria hili la serikali tatu ni bora kujibu maswali mengi sana yatakayojitokeza huko mbeleni.  

Na pia wamesema kila nchi itaruhusiwa kujiunga au kujiondoa katika mashirika ya kimataifa ipendavyo. Sasa kama kila nchi itaruhusiwa kufanya hivyo na katiba ya muungano inasema mwakilishi wa Tanzania katika mambo ya nje ni raisi wa jamuhuri ya muungano hii kweli inamake sense?  Ina maana mfano Tanzania Bara imejiunga katika shirikisho fulani na raisi au viongozi wa jamuhuri ya muungano ndio wataenda kuwakilisha huko hivyo Zanzibar itaingia gharama za kusupport shirikisho hilo bila kupata faida yeyote? je kama Zanzibar wakijiunga na shirikisho aabalo tanzania bara haiamini misingi ya hilo shirikisho haitakua kusupport kitu ambacho hawakiamini? Je kuna usawa kweli hapo? Na kama shirikisho walilojiunga upande mmoja hawakubaliani nalo itakuaje?

Katika kipengele cha hela wamezungumzia kwa ufupi sana na kuachia bunge majukumu. Ni bora kuingiza mambo ya msingi katika katiba kama bunge likitunga sheria huko mbele itakua kuongezea au kubadilisha kutokana na wakati huo kama inahitajika. Lakini wakati huu ambao wananchi wanapewa direct voice ya kutengeza katiba ni bora kuingiza mambo yote ya muhimu. Hela ya jamuhuri ya muungano ni ipi? Benk kuu ya jamuhuri itashughulikia hela gani? Je kutakua na hela tofauti kwa kila hizi nchi na hela ya muungano pia? Nini adhabu ya mtu akitumia hela ya nchi nyingine nchini Tanzania? Kwa sababu kwa mtindo uliopo sasa hivi Tanzania wa watu wanalipwa kwa kutumia tshs lakini wanajikuta wanalipia huduma mbalimbali wakiwa ndani ya Tanzania kwa kutumia US$, hiyo ni uonevu kwa wananchi wa hali ya juu. Serikali ni mtetezi wa wananchi hivyo inatakiwa kuangalia hii na pia serikali ni mtetezi wa hela ya nchi yake kwa kuruhusu hela za nchi za kigeni kutumika nchini ni kuzidi kuishusha thamani ya hela ya Tanzania kwa sababu mahitaji yake yanakua yanapungua. Sasa katiba inasema nini kuhusu hilo?Bunge lina maslahi yake ndio maana mpaka sasa hivi wala hawajali wakiona hela ya US$ inatumika katika huduma nyingi za nchi. Hivyo sasa hivi katiba ya nchi imkomboe mwananchi wa kawaida.

Jaji mkuu, makamu wa jaji mkuu na majaji wa mahakama kuu mimi naona wateuliwe na raisi lakini bunge liwachunguze na kuwakubali. Hivyo kwavile kila kipindi cha kuongeza jaji mwingine kitachukua muda mrefu sana basi kusiwe na ukomo wa umri. Jaji akichaguliwa na akapita basi iwe mpaka kufa, kujiuzulu au kuondolewa kwa makosa fulani. Hiyo itasaidia kuwa na waadilifu, itapunguza muda wa kuchagua jaji wengine kila mara na pia kwa mtu anayejitunza vizuri miaka 70 ni mdogo sana bado wisdoms zake zinahitajika katika taifa sana tu.  Na pia kusema wasiwe wanachama wa chama chochote sio jambo zuri na pactical sio kweli. Ni bora kujua sera zake ni zipi hadharani. Sasa ina maana mtu akihisi kuwa kuna siku atachaguliwa kuwa jaji hivyo aache kuwa na chama au kufuata sera za chama fulani?  Utafahamu mtu utu wake kwa chama anachokifuata kinasimamia sera gani. Kwa vile hao majaji watakua wamaisha basi raisi mwingine akiingia itabidi ajifunze kufanya kazi na majaji ambao waliteuliwa na raisi mwingine hata kama wanafuata chama chake au la. Hiyo ndio demokrasia ya kweli.

Wakuu wa mikoa/Wilaya kuepuka kushughulikia hili jambo katika katiba hii ni kuirudisha nyuma zaidi Tanzania kimaendeleo. Wakuu wa mikoa na wilaya kwa njia hii wanayoteuliwa hawafanyi kazi kabisa kwa ajili ya mikoa yao bali kwa kulinda kazi zao. Hivyo wengi wao watakubaliana au kupingana na wananchi kwa jambo lolote kwa kusikiliza sauti ya boss wao. Na hata kama kuna jambo walikua wanataka katika mikoa yao once raisi akisema no wao wanakua hawana jinsi bali kukubaliana naye ili walinde kazi zao. Na kama kuna jambo wanajua kabisa halitasaidia maendeleo ya mkoa wao lakini once raisi akisema yes basi wanakubali ili kulinda kazi zao. Na pia kama tunavyoona kila siku hawa watu wakiharibu au wakionekana hawajafanya kazi mkoa/wilaya fulani wanahamishiwa sehemu nyingine bila kujali manufaa yao katika huo mkoa/wilaya ni yapi. Imefika sasa wakati wa kubadili hii system ya kuwateua viongozi hawa ili waweze kufanya kazi zaidi ya kuleta maendeleo katika mikoa yao kuliko kulipwa tu bila kufanya lolote na kuwaachia mambo yote ya maendeleo wabunge. Ni bora hawa wakuu wa mikoa/wilaya wakachaguliwa na wananchi sasa.

Na kama spika wa bunge la muungano asiwe mwanasiasa so be it lakini wa Tanzania Bara ni lazima awe mwanasiasa.  Kusema spika wa bunge na naibu wasiwe wanasiasa hiyo ni kujidanganya na itaongeza indirect corruption na unafiki. Spika atakua na chama chake anachokipendelea au kurubuniwa na supporters wa chama fulani lakini mbele ya macho ya watu anaweza kujifanya yupo neutral. Spika wa bunge awe anatoka kwenye chama chenye wabunge wengi katika kipindi cha bunge bila kujali raisi anatokea katika chama gani. Na ili uamuzi wake akiutoa watu wanajua fika ameutoa kwa vile yeye ni mwanachama wa chama fulani.

Kwa upande wangu uraia ningeona ni vizuri kuweka uraia wa Tanzania unapatikana kwa njia hizo walizozielezea kama mtoto huyo anazaliwa nje ya nchi lakini kila mtoto anayezaliwa nchini Tanzania kama wazazi wake hawako nchini kwa kufanya kazi za kidiplomasia basi hao watoto waruhusiwe kupata uraia kama wazazi wao watapenda. Wakifanya hivyo wataisaidia sana Tanzania miaka ya huko mbele. Kuna talents nyingi zitapotea sana kwa kuacha kuwapa uraia hao watoto.Uraia wa tanzania uwe by birth..Ikiwa na maana ukizaliwa kwenye ardhi ya tanzania automatic unakua raia wa tanzania iwapo kama wazazi hawatataka awe raia wa nchi wanazotoka. Mtoto akifikisha miaka 18 ni lazima kupata passiport ya Tanzania au ya nchi wazazi wake wanayottoka kwa vile Tanzania haina uraia wa nchi mbili.

Wabunge wakuteuliwa waondolewe iwe hii ni katiba ya muungano au ya Tanzania bara. Nini faida ya kuwaweka tena hao wabunge kama mawaziri watakua wanateuliwa? Mawaziri wakiteuliwa watakua wa sehemu zile ambazo hawa wabunge wa kuteuliwa walikua wanateuliwa ili kujaza hizo nafasi. Hawa wabunge wakuteuliwa hawafanyi kazi kuwawakilisha wananchi kama vile walivyo wakuu wa mikoa na wilaya bali wanafanya kazi kwa kuwalinda waliowateua. Wabunge wa majimbo huwa wanawakilisha wananchi wote bila kujali jinsia zao, umri wa wao au hali zao. Hivyo imefika muda wa kuodoa wabunge wa kuteuliwa Tanzania.

Na pia ni vizuri kama walivyoweka mawaziri wawe at least na shahada na ujuzi wa idara wanazokwenda kuzitumikia ni muhimu lakini kitendo cha kuweka kuwa rais awe na sahada ni kukiuka misingi ya usawa katiba inayoizungumzia. Naelewa miaka inavyokwenda kila mtu anayetaka kugombea uraisi atakua na shahada lakini kwa kuweka hivyo kwenye katiba hapo wanavyofanya ni kuwa yule mtoto anayezalliwa katika familia masikiri hana right sawa na yule anayezaliwa kwenye familia ya wazazi wanaojiweza ambayo yeye guarantee atakwenda kupata shahada iwe amefell au la. Si tunaona wengi hawafanyi vizuri na bado wazazi wao wanawapeleka nchi za nje kupata shahada? Je mtoto wa masikini ni ipi nafasi yake ya kulitumikia taifa lake? Kwanza shahada sio bure Tanzania kama miaka ya nyuma kama watatoa shahada hiyo bure basi ni sawa kwa vile hapo kila mtoto ana chance ya kuipata hiyo shahada na ni juhudi zake na bidii za mtoto huyo ndio zinatoafutisha hapo na sio hela. Raisi wa nchi kigezo cha sijui shahada lazima kiondolewe. Kwanza elimu haihusiani na uongozi bora.  Kama ingekua hivyo basi Tanzania ingetakiwa iwe na maendeleo sana sana kuliko hata USA kwa vile ukiangalie elimu walizo nao bunge la Tanzania na House of representative ya US kwa asilimia bunge la Tanzania linazidi kwa elimu. 

Universal education. Ukiangalia sasa hivi Tanzania kuna system nyingi sana za elimu. Katiba haijaweka elimu ya Tanzania iwe ya mfumo upi kwa kufundisha. Bila kuweka kwenye katiba elimu ya Tanzania ni ipi ndio kunaendelea kuwa na matabaka mengi sana na watu kujikuta wakitoka lets say form six wakienda kufanya advance diploma ni repetition ya mambo mengi iwapo wanachukua mfumo fulani. Hivyo ni heri kuweka std kama ni America system shule zote za Tanzania zifuate hiyo na kama ni European system basi iwe kwa kila shule hata kama ni ya serikali au private. Na vyuo vya juu navyo viweke curriculum zao kufuata za elimu za chini ili kusaidia wanafunzi kutolipa hela na kurudia rudia vitu hivyo hivyo tena bila kuwa credited cheti cha maana. Hiyo ni kupoteza hela na muda wa watanzania wengi.

Kila jimbo liwe na wawakilishi wawili ni sawa lakini hii ya kuweka kuwa ni lazima mmoja awe mwanamke na mwingine awe mwanamme naona hilo limepitwa na wakati. Kuna wanawake wengi sana wana elimu na ujuzi kama wanataka kuingika katika kazi hii ya kulitumikia taifa kwa kuwa wawakilishi basi waingine na kugombania kama wanaume. Nchi ikiwa bado inapeleka watu kwa ajili ya jinsia katika mambo ya kupigiwa kura sio kulisaidia taifa. Ni kuonyesha kuwa bado wanawake ni wadhaifu na hiyo inazidisha hata akili zao kufikiria hivyo. Ulimwengu wa leo umekua mdogo sana hivyo ina maana kuna watu wengi watatoka Tanzania na kwenda kuishi nchi nyingine. Sasa kuwalea lea wanawake kwa kuwapa priviledges na favoritisms  kwa ajili ya jinsia wakienda kushi nchi nyingine watashindwa kuishi kabisa kwasababu wamezoea kuwa favored. Usawa wa kila mtu uwekwe na kujulikana katika sheria. Zikishawekwa vizuri na kuhakikisha zinafuatiliwa basi hakuna tofauti kati ya mwanamke na mwanamme katika ulimwengu huu kiutendaji. Wakifanya hivyo kuna wanawake wengi wataingia bungeni kwa ajili ya jisia zao lakini kazi hawaijui je hiyo itamsaidia vipi mtanzania wa kawaida? Au inamfundisha nini yule mtoto wa kike? Ina mfundisha kuwa kwa ajili ya jinsia yako hata usipojitahidi sana unaweza kupitishwa pitishwa tu katika sehemu nyingi tu. Hilo sio somo zuri kwa mtoto wa kike wa kitanzania. Wawakilishi wawe wawili na it doesn't matter kama wakiwa wote ni wakiume au wote wakike as long wamechaguliwa kihalali. 

Haki za mfungwa zionyeshwe kimaandishi kuwa ni siku ngapi mtu anaruhusiwa kukaa jela bila kufunguliwa mashtaka. Walivyosema “mapema’ katika lugha ya sheria hiyo inaweza kuwa na maana nyingi sana. Wakisema "afikishwe mahakamani mapema" inaweza kuwa week, mwezi au hata mwaka kwa mwingine ataita hiyo mapema. Kama mtu amewekwa jela iwekwe sheria kuwa ni masaa 48 au 72 au week tu kama waliomshika wameshidwa kutengeneza kesi yao basi aachiwe na iwe hakuna kama wamemfungulia mashitaka haraka haraka na wakashindwa kuprove basi iwe hakuna kumshika tena kwa kosa hilo hilo. Hii itapunguza hata idadi ya watu walioko jela ambao wanashikwa tu bila sababu ya msingi na kuweka jela bila kufunguliwa mashitaka kwa muda mrefu sana. Na wakati mwingine police au watu waliowashitaki wanakua hawana kesi ya maana bali uonevu wa watu hivyo watu wanakaa jela tu na katiba haina mahali inapoonyesha kuwatetea. Na itawafanya wajue kuchunguza kitu kabla ya kukimbilia kumweka mtu jela na mwishowe wanakua hawana kesi wanaishia kumwachia mtu. Huo ni uonevu wa haki za watu. Kuwe na muda kamili na uonekane kwenye katiba.

Pia hawajaonyesha sheria ya kuchukua, kumkamata mtu au kusearch properties za watu kama nyumba, gari na sasa hivi simu. Iwe kuna sheria kama mtu akikubali kusechiwa katika nyumba yake ni sawa lakini kama akikataa police lazima wawe na searching warrant kutoka mahakamani unless wanachokisearch haraka hivyo kinahatarisha usalama wa taifa. Sio kuingia tu kwenye nyumba za watu na kusearch bila kujua wanatafuta nini, kukamata watu bila kujua wanaowakamata ni watuhumiwa waliokua wanawatafuta kweli au la na kuchukua mali za watu bila idhini yeyote. Hilo nalo ni muhimu kuonyeshwa kwenye katiba.

Viongozi wa umma kuonyesha mali zao na za watoto wao wasio na umri zaidi ya miaka 18 ni vizuri lakini wangeweka watoto wao wote bila kujali wana umri gani kwa vile wengine watapewa vitu na wazazi wao na kujifanya kuwa wamejitengenezea wenyewe. Au watapewa contract na watu wanaofanyiwa favor na baba yao na kutajirika haraka haraka ila ukweli unaojulikana kuwa kila kitu sio halali lakini hamna mtu wa kusema kwa vile hakuna sheria. Wakati mwingine muda wa utajiri huo haulingani na muda wa huyo mtoto alivyoanza kufanya kazi hivyo ni bora wote waonyeshe na jinsi walivyojiingizia hiyo hela kila mwaka. Hiyo ndio price to pay ya mzazi akishaamua kuingia kwenye utumishi wa umma. Afahamu kuwa kuchagua kuwa mtumishi wa umma ni wito na pride kwa familia yake na vizazi vijavyo na sio kujipatia utajiri wa haraka haraka. Na itawafanya kabla ya kukimbilia uchu wa uongozi waweze kukaa chini na familia zao na kuwashirikisha katika maamuzi ya kutaka kuwa mtumishi wa umma. Faida na hasara zake na watoto wake wote wawe wanajua watakua kwenye kioo cha umma.

Kodi ni zipi? Na ni nani anatakiwa kulipa kodi? Ingetakiwa kila raia wa Tanzania mwenye kufanya kazi lazima alipe kodi ya jamhuri ya muungano regardless of where he/she lives. Hata kama ni cent moja kuchangia kitu ni muhimu sana. Inampa mtu sauti zaidi na moyo wakufuatilia mambo ya nchi kwa vile anajua hela yake inachukuliwa. Huu ni muda wa kuweka kuwa kila mtu anayeishi Tanzania kwa kipindi cha mwaka mmoja na kuendelea aonyeshe kwenye department ya treasury kuwa ametengeneza shilingi ngapi kwa mwaka ule na amelipa kodi shilling ngapi. Kama nchi inataka maendeleo inatakiwa ianzie kwenye katiba. Kila mtu mwenye umri wa kufanya kazi aonyeshe. Itasaidia kwa upande wa wananchi na upande wa serikali pia kuweza kukusanya kodi. Na kila mtanzania anayefanya kazi nje na ndani ya nchi basi kama ametengeneza zaidi ya kiasi fulani ( iwekwe kwenye katiba) basi alipe ushuru. Yes itaoneka kuwa hii haitawezekana lakini hakuna jambo lisilowezekana. Litachukua muda lakini inawezekana.

Katika jeshi la wananchi wamesema tu jeshi la wananchi wa Tanzania lakini Jeshi la Polisi wamesema ni jeshi la police wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania? Hizo lugha hapo ni tata. Bora kieleweke. Isije kuwa jeshi la wananchi la Tanzania likalipwa na Tanzania bara lakini likatumika kulinda jamuhuri ya muungano…Ni heri waandike kila kitu kieleweke kuwa ni jeshi la wananchi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania. 
 
Pia wanavyosema kila mtoto ana haki ya elimu lakini hawajaweka umri wa legal wa kuwa mtoto ni upi Tanzania? Tunaona kila siku watoto wana miaka 12  to 16 wanasimamishwa shule na wazazi wao na kuozeshwa. Legal age ya mtoto Tanzania inatakiwa kuonyeshwa. Na hiyo haki ya elimu anayotakiwa kupatiwa ni ya mpaka elimu ipi ijulikane. Iwekwe kwenye katiba ili ijulikane kabisa na sheria hii itasaidia kumprotect watoto Tanzania .

Na pia wakisema kila mtoto ana haki ya kupata malazi na chakula je ninani anatakiwa kutoa hayo? je ni mazi au serikali. Ni bora iwekwe ili hawa watoto wa mtaani ijulikane ni nani wa kushitakiwa. ongezeko la watoto wa mitaani ni kwa vile hakuna mtu wa kushikwa katika hili. Serikaliinatakiwa kuweka kwenye katiba mtoto (umri uwekwe) asipopata hayo basi mzazi anashitakiwa. hii itawafanya wanaume na wanawake pia wawe wanafikiria mara mbilimbili kabdla hawajaamua kuzaa mtoto. 

Neno umri halijawekwa katika katiba..imewekwa kila kitu kama bila ubaguzi wa rangi, kabila, jinsia, na dini lakini hawajaweka umri. Inatakiwa watu wawe protected kwa umri kwa vile kuna age discrimination sana sana Tanzania na hakuna mtetezi wa hilo. Kila siku unaona wameweka kwenye ajira mtu asizidi umri fulani. Hiyo ni age discrimination na inaonyesha katiba imeachia mwanya ili hilo liendelee tu nchini.  Kama ni equal right for everyone wasingeweka hayo hapo juu ya rangi, kabila, jinsia na dini wangeacha wazi ili kila kitu kiwe ni agaist the law kama mtu akibagua. Lakini kuweka hayo mengine na kuacha umri ni kuongeza mwanya wa ubaguzi nchini Tanzania. 

Mambo kama legal marriage ni ipi Tanzania. Sasa hivi tunaona ulimwengu unavyobadilika mambo mengine yakiachwa kwenye katiba ni kutojitahidi kutunza misingi ya Tanzania. Je katiba inasema nini katika ndoa za watu wa jinsia moja? Kama haisemi chochote ina maana inaruhusu? Na je hao watu wa jinsia moja wakioana na wakiachana katika kugawana mali etc ni nani atakua mtetezi wao? Ni bora kuonyesha misingi ya Tanzania katika hili.  

Pia Tanzania kuna ndoa hasa za kiislamu kuwa wanaruhusu mtu kuoa wanawake zaidi ya mmoja je katiba ya nchi inasemaje kuhusu hili. Kama inaruhusu basi iweke hadharani kuwa katiba ya Tanzania inaruhusu one to many au many to one...weka katiba. Kuacha hivyo ina maana watu wenye dini ya kikristo ndoa zao ni one to one, wenye dini ya kiislamu ni one man to many women. Na je wasio na dini itakuaje? Je ni legal Tanzania kwa mwanamke mmoja kuolewa na wanaume wengi pia? Kwa vile katiba hajasema chochote kuhusu hili ina maana anything goes. Siku mwanamke akiolewa na wanaume wengi atakua na haki sawa sawa katika kila mume kama yule aliyeolewa na mume mmoja au katika ndoa yenye mwanamke zaidi ya mmoja. Katiba inatakiwa kusema haya wazi bila kuachia dini na mila za jadi kuamu.

Rights za wazazi hawajaziweka pia. Tunakoelekea ni bora kuweka right za wazazi kwenye katiba. Watoto wa siku hizi hawakui au hawaonyeshi kupenda kujitegemea bali wanakaa nyuma kusubiri wachukue vitu vya wazazi wao na pia hawawatunzi baada ya kuwafilisi kila kitu au kuspend kila kitu cha wazazi wao. Ni bora kuweka haki za wazazi.  Pia wazazi wanawajibika kuwatunza watoto wao mpaka miaka mingapi kisheria. Bila kuweka hili ndio tunaona watu wengi wanazaa na kuacha watoto wao tu mitaani wateseke. Kuachia jadi na mila ni kuendelea kuachia wengi wateseke. Haki za wazazi zieleweke na mtu akizaa mtoto ajue sheria inamshika katika kutunza huyo mtoto mpaka afikie umri fulani.Hii pia itasaidi akupunguza umasikini Tanzania kwasababu watu watakua wanafikiria kabla ya kukimbilia kuzaa zaa tu na kuachia bibi na babu au ndugu watunze yule mtoto. ni bora katiba iseme kabisa.

Adoption, katiba inasemaje kuhusu hii. Kuna wengi tunajua jinsi ilivyo na uchungu unapochukua mtoto wa mtu wakati akiwa na shida na kumtunza na kumfanya wako. Mara anapokua anaendelea vizuri mara familia za yule mtoto anapotoka zinakuja kumchukua mtoto wao bila hata kuangalia mtu kwa kukaa na yule mtoto umeinvest kiasi gani financial au emotional. Lakini kwavile hakuna sheria katika katiba katika hili basi mtu unaishia kumwachia yule mtoto. Iwekwe sheria kuwa mtu akitunza mtoto wa mtu hata kama hawajaandikiana mahali lakini akikaa naye kwa muda fulani (muda upangwe) basi anakua mtoto wake kabisa. Na hakuna mtu kuja kumchukua huko baadaye. Wao ndio wanakua kama wazazi kabisa wa huyo mtoto na kuwa chini ya sheria kudaiwa kumsomesha. Sio hii unatuza mtoto kama ni wa kike wanandugu wa huyo mtoto wakishaona amekua binti sasa wanajidai kuja kumchukua ili waendelee kumtunza kumbe wanataka wakamwozeshe ili wapate mahari. 

Na jambo la uzazi ni bora kulianhgalia. Huko tunakoelekea kuna mambo ya surrogate mothers’ yatakwenda Tanzania. Je wamejiandaa vipi katika mambo haya na right ni zipi kwa hilo Tanzania. Wengi wataingizwa kwenye hizi biashara bila kujua haki au sheria zao ni zipi. Wengi watatumia wanawake hao na kujikuta wanalipa mara nyingi na mwisho wa yote hawampati huyo mtoto. Weka kama mtu wamekubalina kufanya hivyo nini rights zao? Na huyo mtoto akizaliwa atakua raia gani?

Katiba inasemaje kuhusu mambo ya mirathi? Wamesema kwenye katiba ardhi ni muhimu Tanzania na kama biandamu wote ni sawa. Je katiba inasemaje kuhusu hili. Kama mtu akizaa watoto wengi na wengine nje ya ndoa, je hao watoto hawana haki ya kurithi chochote kwa baba yako hata kama walikua watoto wa nje ya ndoa? Ni muhimu kuweka haki zao katika katiba. Kuna watoto wengi sana wanaishia kuteseka wakat baba zao walikua na hela nyingi sana za kuweza kuwatunza. Hao watoto hawakuomba kuzaliwa katika mazingira hayo na wala kosa sio lao hivyo serikali inatakiwa kuwatetea katika hili. Weka kila kitu kijulikane kuliko kuiachia jamii na mila.Tunaojua jinsi watoto wa kambo tena wakiume wanavyobaguliwa. Siku hizi kuna DNA unaweza jua kabisa kuwa huyu ni mtoto wa mtu fulani kiurahisi sana na sio kusema sikutambuishwa wakati akiwa hai. Sheria ziwekwe kuwalinda hawa watoto, wanawake, watoto wa kambo, watoto wa kike etc. 
Ni muda wa kuondoa posho kwa watumishi wa uma. Kutumikia umma ni wito na mapenzi ya mtu kwa nchi yake. Wako wengi wangependa kufanya kazi hiyo kwa moyo wote bila hata posho. Hivyo ni muda wa kuondoa posho serikalini. Kwanza posho ni hela ambayo ni kama rushwa. Hawailipii kodi na wala huwezi jua mtu huyu kapata ngapi kwa mwaka. Hivyo ni bora kuput kila kitu katika mshahara. Marekani nchi kubwa kama hii lakini hawana posho na wawakilishi wao mara nyingi wanaamua kuwaacha familia zao katika majimbo yao na wakiwa Washington DC wakati wa vikao wanaamua kushare nyumba na wawakilishi wengine na wengine wanaweka makao katika office zao ili kusave hela. Kwa vile hawana posho za hivi wala vile kama Tanzania wakati wao wana nchi yenye uchumi wote huo na nchi yao haitegemei msaada kufeel gab ya budget yao.  Benefits wanazopata ni kama za wafanyakazi wote wa serikali.  Kuweka posho katika katiba sio halali kabisa. Utumishi wa umma ni sacrifice na mapenzi ya mtu kutumikia taifa na sio kujitajirisha na posho. Na ukiweka hivyo utajua kabisa ni nani anapata hela nje ya rushwa na kujitajirisha kwavile utajua mishahara yao ni kiasi gani. Hivi sasa wengi wanatajirika haraka haraka na kusingizia kuwa posho zao hawaitumii bali ni kusave na kufanya hayo mambo. Ondoa posho kwa viongozi wa umma. Kila mfanyakazi anafanya kazi kwenye mazingira magumu Tanzania. Watumishi wote wa umma basi wapewe posho na sio wa ngazi za juu tu kama ni hivyo.

Pia hawajaweka haki za mfanyakazi Tanzania.  Katiba inatakiwa iseme yote yatakayomsaidia mfanyakazi yeyote na kuacha kuwa watumwa nchini mwao. Masaa ya kufanya kazi kwa week yaeleweke na baada ya hapo ijuilikane ni overtime. Hii itasaidia hata wafanyakazi wa ndani wanaotumikishwa kama punda, hawapumziki na msahara sio mwingi. Maendeleo ya nchi yanapatikana pale serikali inapowalinda wafanyakazi wake. Umri wa kufanya kazi ni bora ujulikane kwenye katiba pia. Itasaidia kupunguza underage workers. Watu wanaowafanyiza kazi watoto hao hawawalipi vizuri na pia wanafanya wasiende mashuleni.   Na hii inakwenda na wakulima na wafugaji haki zao ni zipi?  Tunajua uti wa mgongo wa nchi ni wakulima je wao wanakua protected vipi kwenye katiba ya nchi?

Sheria za watu kuwa na bunduki ni zipi? Katiba inasemaje kuhusu hili? Nani anaruhusiwa kuwa na bunduki Tanzania na nani haruhusiwi? Ni bunduki za aina gani zinaruhusiwa kwa raia? Je watu ambao sio raia wa Tanzania wanaruhusiwa kuwa na bunduki wakiwa nchini? Katiba ionyeshe kabisa katika usalama wa taifa.

Haki za mteja nazo ni zipi (consumer rights)? Zinatakiwa zionyeshwe kabisa kwa sababu quality zimepungua sana za bidhaa na huduma. Utapeli umekithiri Tanzania.hakuna haki za mteja kabisa. Zikiwekwa hizi kwenye katiba hata wauzaji au watoa huduma hao wataweza kufanya kila kitu kwa umakini na hata mashirika mengi yatabidi kuwahamasisha wafanyakazi wake kujua kutoa quality products au services kwasababu inajua kama sheria ya nchi inawalinda wateja basi wao ndio watakua sued kwa kuwaachia hayo yafanyike katika mashirika yao. Watu wanakufa kila siku na ajali a mabasi lakini hakuna kinachoendelea zaidi ya watu kupotea ndugu zao na wafanyabisahara zao kuendelea kutajirika tu. 

Na mimi swali langu baada ya hayo yote ni hili kama hapo wanaposema mtoto ana haki ya kupata malezi bora na elimu. Je baada ya hii katiba kuanza kutumika kwa mfano wazazi wa watoto wa mitaani watashitakiwa au ni serikali itatakiwa kutunza hao watoto na kuhakikisha wote wanaishi kwenye mazingira mazuri na kwenda shule? Kwa sababu ukishaweka hiyo right katika katiba ina maana mtu asipofanya hiyo basi amevunja sheria za nchi hivyo ni nani atakua responsible hapo?

Mtu ambaye haisaidii Tanzania kabisa ni yule anayekubali jambo au kukataa jambo bila kuwa na sababu yeyote na yule mtu ambaye hajishughulishi kusoma katiba hii mpya anakaa tu kusubiri viongozi wasome na kuijadili halafu yeye anakubaliana na maoni yao kwa viletu ni mpenzi wa chama hicho. Watu hao ni JANGA kubwa sana la taifa. Kama wewe ni mmoja wa hao jaribu kuanza kutumia akili yako uliyopewa na Mungu, kutumia haki yako uliyopewa na nchi  na utaona maendeleo ya haraka katika maisha yako, ya watoto wako na ya vizazi vijavyo.  Remember If you don't stand for something, you'll fall for anything. 

Haya ni maoni yangu tu ..........I hope na wewe una yako....je maoni yako ni yapi? Natumaini watu watazidi kuchambua katiba hii na yakiwekwa pamoja kuna uhakika wa kupata katiba Tanzania inayokwenda na wakati kwa manufaa ya wananchi wote na vizazi vijavyo...

Mungu Ibariki Tanzania







No comments: