Thursday, January 12, 2012

Are you up to virtual freelance jobs?

Hili swali ni kwa watu ambao wamesomea technologia na wanaishi Tanzania. Je mnafahamu hizi site za freelance ambazo sio lazima uishi kwenye nchi nyingine?  Virtual freelance ni nzuri na itakusaidia sana kwa kujiajiri. Site kama Guru.com na Elance ni nzuri sana. Ukianaglia watu walioweka portfolio zao huoni hata nch i ya Tanzania. Je ni kuwa hakuana watu au watu hawajui?

Kama una ujuzi kama katika mambo mbalimbali kama Web programmer, Web Development, Web Design, Flash & Web Animation,  Search Engine Optimization, Visual basic programmer,/ Developer etc etc hizi site zitakusaidia sana. Na ukumbuke sio high tech tu hata kuandika (writer), proof reading, editing,


Jaribu kupita na kutengeneze portfolio yako na ujitangaze kwenye hizo sites...Huwezi jua utatengeneza $ ngapi kwa mwezi au mwaka..Ila cha kujifunza na kuzingatia ni kutolipua lipua... Kama unataka kupata kazi na kupata references kupitia watu uliowafanyia kazi basi ufanye kwa umakini. Kazi unayopata ujue kweli unafahamu kuifanya. Ujue kweli utafanya kitu ambacho mtu anayekupa atafurahia. mambo ya kudanganya kuwa unajua na kuweka portfolio ya uongo na kufanya kazi isiyo na quality sio hivyo. Huku watu wanacharge back credit card zao kama kazi uliyowafanyia haifananai na walivyotaka.

Na usiwe na tamaa ya kucharge kama unaishi USA..Just jitahidi kuangalia watu ambao wanaishi nchi kama India na zingine uone wao wanacharge vipi. Nakumbuka mwaka 2009 kuna kazi nilikua natakiwa kumaliza lakini na mtoto mcahnga ilikua shida sana kuifanya na kumaliza on time..Nikaingia kwenye site ya Tanzania moja nikapost nilichokua nataka..Watu wote walinijibu walitaka $250 na $350. Nikaweka hapa kwa craiglist nikapata mtu aliyenifanyia kwa $50. Sasa nikawaza ni watu wanagapia wanapoteza nafasi za kurengeneza portifoli zao kwa ajili ya kutojua kuprice kazi zao? Ni tamaa ya kutaka kuwa tafjiri haraka haraka au ni kutokujua? Au kufikiria kwa vile mtu yupo nchi fulani basi ngoja ni mchomoe. Lakini ukiwa unafanya hivyo hutapata mtu....Jaribu kuweka kile unachotakiwa kufanyika kwa gharama za kawaida. Kumbuka watu wako wengi wenye ujuzi kama wako na siku hizi kwa internet inakua rahisi kucompare. 

Na pia ukitaka kujijengea jina vizuri hakikisha muda unaowapa ndio utakao maliza kazi yao kweli. Mambo ya njoo kesho hayapo huku..Kama mtu anataka kazi yake ifanyike kwa siku tatu na wewe unajua kabisa hutaweza kwa muda huo ni heri umwambie ukweli na kama hataki basi uiache. Huku contract  ndio inayokulipa au itakayokulipisha. Sasa soma kila kitu mtu anachohitaji na ukikubali ujue unakubali kuwa utaweza kufanya hiyo kazi kwa muda unaotakiwa na quality inayotakiwa...

Sasa kama huzijui hizi sites jaribu kuzipitia Guru na Elance...Najua zitakuwa zipo nyingi lakini mimi  niko familiar na hizi mbili. Kama unajua nyingine basi weka kwenye comments ili wale wenye kutaka kufanya freelance waweze kuziona...

Tuko pamoja and Yes #TUNAWEZA