Wednesday, August 10, 2011

Ugonjwa wa wasiwasi na hofu

Wasiwasi ni jambo la kawaida kwa hisia za binadamu anazokutana nazo katika maisha lakini baada ya wasiwasi na hofu kuendelea na kuwa inaingilia jinsi mtu anavyoishi kila siku basi hiyo ni dalili kuwa ni ungonjwa wa wasiwasi na hofu. Na kama isipojulikana mapema na kutibiwa mapema inawenza kumfanya mtu kuchanganyikiwa. Na hii inawapata wanawake zaidi kuliko wanaume.

Kuna matibabu bora sana ya huu ugonjwa ambayo ni pamoja na dawa au therapist.



Sababu zinazosababisha ugonjwa huu:-

Sababu kamili hazijajulikana vizuri ila mara nyingi ugonjwa huu ni
1. Kurithi
2. Mazingira
3. Kemikali katika ubongo
4. Trauma au kupoteza mtu wa karibu


Dalili za ugonjwa wa wasiwasi na hofu
Hii ni hofu inayotokea bila onyo.
-Moyo unakwenda kwa kasi
-Nguvu zinaisha, kizunguzungu au kuzimia.
-Kufa ganzi na kuwakwa waka kwenye vidole vya mikono.
-Wasiwasi kuwa unakupa au unasubiri kufa tu.
-Kutoka jasho au kusikia baridi.
-Muamivu ya kifua
-Kushindwa kupumua.

Jinsi ya kudhibiti
Ukiwahi kutibu ugonjwa huu mapema ni vizuri sana na jinsi unavyochelewa ndio jinsi itakavyochukua muda kupona.
Dawa
Relaxation
Hypnosis
Therapist