Wednesday, August 10, 2011

Maandalizi kabla hujapata mimba....Je unajua nini cha kufanya kuuandaa mwili wako kabla hujapata mimba?

Unapofikiria kupata mtoto kabla hujapata mimba ni muhimu kuandaa mwili wako na kuzingatia mlo bora.Yako mambo mengi ya kufanya ili ujauzito wako usiwe na matatizo mengi au kama wewe umejaribu kupata mimba kwa muda mrefu bila ya mafanikio ni bora kuuandaa mwili wako vizuri pamoja na mwenzi wako. Kusema ukweli, unapaswa kuanza miezi mitatu hadi mwaka mmoja kabla ya mimba ili kuhakikisha kuwa hali yako ya lishe ni bora. Pia unatakiwa usiwe mnene sana au mwembamba sana. Kumbuka ukiwa na mimba sio wakati wa kufanya diet...

1. Punguza uzito kama wewe ni mnene au kama ni mwembamba sana jitahidi kula ili upate uzito unaostahili.


2. Kama unavuta sigara acha kuvuta.

3. Punguza caffeine..Kama unatumia kahawa au soda zenye caffeine punguza. Imeonyesha kuwa caffeine inasababisha kushelewa au kupunguza nafasi ya kupata mimba.

4. Kuna wataalamu wanasema usile samaki wengi na wengine wanasema shellfish. lakini ni muhimu kujua ni samaki gani na kiasi gani ule kawa siku au week ukiwa unajaribu kupata mimba.

5. Kama unakunywa pombe punguza pombe.

6. Anza kufanya mazoezi kama wewe sio mtu wa kufanya mazoezi.

7. Hakikisha unalala vizuri

8. Punguza stress

9. Mwone daktari wa wanawake

10. Mwone daktari wa meno

Kwa upande wa chakula ili uweze kupata madini yanayostahili ni vizuri ukala vyakula hivi kila siku.

1. Vyakula vilivyo na calcium nyingi mara mbili kwa siku...Kama vile maziwa ya mgando, mtindi, jibini.

2. Kula 7 savings kwa siku matunda na mboga za majani..Yaani mlo wa asubuhi hakikisha unapata tunda, kitafunnio cha asubuhi ule tunda, mchana mlo wako uwe na tunda pia, jioni chakula kiwe na tunda. Halafu mlo wa mchana na jioni hakikisha unakula mboga za majani kwa wingi utakua umetimiza 7 servings per day... Na matunda au mboga za majani jitahidi ziwe na folic acid nyingi kama vile machungwa, dengu, mchicha na broccoli. Na matunda at least uweke yenye vitamic C, kama machungwa, tikiti maji, kiwi na mapapai.

3. Ule 2 savings kwa siku mboga iliyo na protein nyingi lakini haina mafuta kama vile nyama nyeupe ambayo ni nyama ya kuku...

4. Kula mara sita kwa siku vyakula vilivyo na nafaka nzima kama brown rice, oatmeal, na whole wheat bread.

5. Kunywa maji mengi.

Pamoja na mlo mzuri ni vizuri pia ukaongeza supplements (vitamins) Na hakikisha vitamins hizo zina 400 micrograms ya folic acid na 18 milligrams ya madini ya chuma (iron) kila siku... Na kwa mwenza wako ni lazima aongeze vyakula vyenye zinc...Good luck