Wednesday, August 10, 2011
Jinsi ya kupunguza uzito
Usizanie kwa vile wewe umekua mnene maisha yako yote basi hutaweza kupungua. Au kwa vile umeshawahi kujaribisha kupungua na hukupungua basi hutaweza kupungua. Na wengine wanasema ukishakua na umri fulani basi kupunguza uzito sio rahisi. Hiyo sio kweli mtu yeyote anaweza kupunguza uzito iwapo utaishi katika healthy life style.
1, Kwanza ukumbuke ili uweze kupungua ni lazima ulichokiingiza kwenye mwili lazima kitoke. Hivyo kufanya mazoezi ni muhimu sana. Mazoezi ni mazuri katika kupungua au kama unataka kuwa katika uzito wako ulionao sasa hivi lakini hutaki kuengezeka zaidi. Pia mazoezi ni mazuri katika kuweka afya yako sawa. Ili kupunguza kupatwa magonjwa mbali mbali mazoezi sio lazima ufanye kwenye gym au uwe na vifaa vya mazoezi maalumu. Mazoezi unaweza ukafanya bila vifaa vyovyote na ukafanikiwa kabisa.
2. Kama unaweza kupanga mlo wako wa week ni vizuri na uuzingatie . Lakini kama huwezi kupanga mlo wako wa week nzima basi jaribu kupanga mlo wako wa kila siku. Hiyo itakusaidia kujua ni kiasi gani cha chakula unakula kila siku.
3. Jitahidi usiache kula mlo wowote kwa kisingizio cha kupunguza uzito. Watu wote wanao diet na kuacha kula huwa wanaengezeka sana mara wanapoanza kula kawaida. Ili uweze kupungua hakikisha unakula milo mitatu kwa siku na vitafunio viwili kwa siku. Na kama wakati wa kula ukifika huna muda wa kula basi jitahidi hata ule tunda kuliko kutokula kabisa.
4. Maji ni muhimu kwa mtu yeyote. Hakikisha unakunywa maji mengi kila siku.
5. Anza kuwa na tabia ya kuwa unaweka rekodi ya kila kitu unachokula kwa siku na unajua umekula calories ngapi kwa siku.
6. Tafuta MBI (Mass Body Index) Hii ni kipimo cha kuhesabu mafuta uliyonayo mwilini kulingana na urefu wako. Hivyo utajua kama wewe uko kwenye rate inayotakiwa. Na ujue pa kuanzia.
7. Tafuta idadi ya BMR (basal metabolic rate) yako...BMR ni kiasi cha chini cha calories ambacho mwili wako unahitaji kwa siku ili uweze kufanya organs zako zifanye kazi. Hii inakusaidia kujua ni kiasi gani cha calories unatakiwa kula kwa siku. Unaweza ukawa unakula chakula kingi bila makusudi yeyote. Mfano wewe unahitajika kula calories 1300 kwa siku na shughuli zote za siku pamoja na mazoezi basi unaweza kuburn calories 800 kwa siku. Hivyo ili kuuwezesha mwili wako usinenepe basi unatakiwa ule calories 2100 kwa siku Na kama unataka upungue basi ni lazima ule chini zaidi ya hapo kwa vile ukila calories 2250 kwa siku utaengezeka pound 1 kila week mbili.
Vitu vya kubadilisha kwa siku ili uuweke mwili wako kwenye afya nzuri ni kwa mfano
a. Badala ya kunywa coke basi kunywa maji
b. Badala ya kula mkate mweupe kula whole wheat bread.
c. Badala ya kula ugali wa unga wa sembe basi kula ugali wa unga wa dona.
d. Badala ya kuchukua tax kwenda mahali penye umbali wa mail moja au mbili tembea kwa miguu.
e. Badala ya kuchukua lift (elevator) kwenda juu gorofani tumia ngazi.
f. Asubuhi amka dakika 10 kabla ya muda wako wa kawaida na nenda kwa matembezi ya dakika 10 tu (utaburn 100 calories)
g. Badala ya kukaa chini kuangalia TV fanya yoga, pilate, kunyoosha viungo kwa dakika 10 na utapunguza calories 50
h. Kama wewe ni mpenzi wa nyama na bia basi jitahidi upunguze kula au kunywa bia kwa week na utaona mabadiliko makubwa sana.
Na pia there is an app for that... Loose It ni app nzuri sana. baada ya kujifungua nilirudi katika pre pregnancy weight yangu kwa week moja tu. Lakini baada ya kuwa na mtoto anayelia usiku na mchana nilijikuta silali na nikaengezeaka katika mwaka mmoja pound 33. Hii Loose It app imenisaidia mimi kupunguza pound 30 mpaka sasa.