Wednesday, August 10, 2011

Dalili za awali za mimba

Kabla hata hujaanza kutumia vipimo vya nyumbani vya kuhakikisha kuwa una mimba, kuna dalili zingine utaziona mapema. Dalili nyingi ni kama vile siku chache kabla hujapata siku zako.

1. Matiti kuwa magumu na kuvimba. Kwa wengine hata kuuma.

2. Kuchoka - fikiria kama unakimbia marathon bila mazoezi.

3. Kuwa na hamu ya vyakula baadhi na vingine kutovipenda kabisa.

4. Kichefuchefu na kuweza kuwa na hisia za harufu mapema.

5. Kwenda chooni kukojoa mara kwa mara.


6. Tumbo kujaa kama umevimbiwa.

7. Baadhi ya wanawake watapata kuona kama sikuzao kidogo sana. Wakati yai likiwa linajijenga kwenye kwenye ukuta wa uterine.

8.Baadhi ya wanawake pia watapata maumive kama ya kuona siku zako (cramps) kwa week chache za mwanzoni.