Wednesday, August 10, 2011

Jinsi ya kujua Ovulation yako

Jinsi ya kujua ovulation cycle yako..

1. Angalia kalenda yako. Ovulation huwa inatokea katikati ya menstrual cycle yako. Cycle za watu wengi ni siku 28 lakini tokea siku 23 mpaka 35 ni kawaida. Hivyo unatakiwa kujua cycle yako ni siku ngapi. Sio kila mtu ana siku 28 cycle. Wakati mwingine cycle yako inaweza kutofautiana kutokana na mambo mbali mbali kama stress, kuchoka, safari, mazoezi. Hivyo unatakiwa kutrack cycle yako kwa miezi kadhaa kujua normal cycle yako ni ipi... Baada ya kujua hesabu kutokea siku ya kwanza ulivyopata siku zako kama siku ya kwanza... Lakini kama siku zako huwa haziko kawaida mara zote basi ni vizuri kutumia njia nyingine.



2. Sikiliza mwili wako. Kama wewe uko kwenye 20% ya wanawake ambao mwili wao unawaeleza wakiwa ovulate basi jaribu kusikiliza mwili wako. Unaweza kusikia maumivu (cramps),mara nyingi upande mmoja. upande ambao yai lime ovulate.

3. Angalia temperature yako. Lakini hii unawezafanya hivyo kwa kipima joto maalum. uwe unachukua asubuhi kabla hujatoka kitandani na uifananishe kwa miezi kadhaa.

4. Fahamu cervix zako. Katika mzunguko wa cycle yako ile sehemu iko kama shingo katikati ya vagina na uterus ambayo inapitisha kichwa cha mtoto ukiwa unajifungua inakua chini, ngumu na imejifunga. Wakati ovulation inaanza inajivuta nyuma kidogo, inalainika na inafunguka. Wanawake wanaeza kuzisikia hizi tofauti. Check kila siku na uandike observation zako.

5. Nunua ovulation predictor kit kama una uwezo au kama zinapatikana sehemu unapoishi ili uweze kutumia hiyo kukusaidia kujua siku ambayo uko ovulated....

Na pia siku hizi unajua lile tangazo wanasema "there is an app for that" ...yes there is an app for this one too...Nadhani hii app inapatikana kwa platform nyingi...kama una Iphone basi download period tracker app. Ni nzuri sana...ya free ina mambo mengi tu...