Wednesday, August 10, 2011

Jinsi ya kudhibiti kisukari bila madawa

Kama una ugonjwa wa kisukari (type 2) unaweza kudhibiti hali yako bila kutumia madawa lakini sisi wote tunajua kwamba kudhibiti sukari inaweza kuwa changamoto sana. Lengo lako ni kuhakikisha sukari yako ipo kwenye number zinazotakiwa mara kwa mara. Baadhi ya watu kutumia dawa kama tiba ya ugonjwa huu. Lakini kwa kutegemea matokeo ya number zako za kisukari a1c na daktari wako atakavyokuona unaendelea basi wewe unaweza kujaribu kudhibiti ugonjwa wa kisukari yako bila dawa.


Jinsi ya kudhibiti hali yako
1. Moja ya hatua muhimu zaidi unaweza kuchukua ili kudhibiti wewe mwenyewe ni kuangalia viwango vya sukari yako mara kwa mara. Wakati kifaa cha kuchekia damu kinaweza kuwa ghali sana lakini ni muhimu kuangalia ili kuhakikisha kwamba sukari yako iko katika viwano vinavyotakiwa. Na kulingana na viwpimo vyako unaweza kuamua kama mabadiliko utaweza kujua nini kinahitajika kiongezeke kati ya chakula na mazoezi.

2. Njia nyingine kubwa ya kukabiliana na hii ni ya kisukari type 2 ni mazoezi. Mazoezi yanasaidia kurudisha damu yako katika kiwango kinachotakiwa..

3. Kitu kingine cha kuzongatia ni kula chenye afya. Jitahidi kula vyakula vinavyoruhusiwa kwa watu wenye kisukari na ufuate masharti. Hakikisha unakula matunda, mboga za majani na vyakula vyenye protini. Vyakula vyenye Carbs nyingi sio vizuri na daima angalia damu sukari yako kabla na baada ya mlo wowote. .

4. Hivi karibuni imegundulika kuwa mdalasini ina saidia kupunguza sukari. Jitagidi utumie mdalasini katika vyakula unavyokula.

5. Kama unavuta sifgara basi jitahidi uache mara moja.

6. Tumia busara kama wewe ni mnywaji wa pombe. Pombe inakua processed katika mwili sawa sawa na kama vile mwili unavyoprocess mafuta. na pia pombe ina calories nyingi sana. Kama wee unaamua kunywa pombe kunywa tu pale damu yako ipo vizuri kabisa.