Wednesday, August 10, 2011

Jinsi ya kula vizuri ili uweze kuishi na Kisukari bila matatizo

Kula lishe bora ni muhimu kwa kila mtu, lakini kwa ajili ya kisukari, kula lishe sahihi ni muhimu kwa ajili ya afya yako.

Angalia maelekezo haya yataweza kukusaidia kuweka Kisukari katika number zinazotakiwa:-

1. Kula vyakula vyenye nafaka nzima - kama vile ngano ambayo haijakobolewa, Mchele ambao haujakobolewa, Mahindi ambayao hayajakobolewa kila siku. , Matumizi yote-nafaka na chakula kwa toast na sandwiches; mbadala brown mchele kwa ajili ya mchele nyeupe kwa ajili ya nyumba milo kupikwa na wakati dining nje.



2. Kula matunda na mboga za majani kwa wingi. Kama maganda ya matunda hayo yanaliwa basi ni vizuri ule kuengeza fiber katika mlo wako.

3. Ili kupata protin ni muhimu kula vitu kama kunde, maharage, mbaazi na dengu lakini kama unakula nyama basi kula kwa wastani na sana sana ule samaki, kuku na kama ni nyama nyekundu (red meat), basi jitahidi kula ambayo haina mafuta (lean meat).

4, Hakikisha unakunywa maji kwa wingi. Kila mahali unapokwenda hakikisha unachupa ya maji na unakunywa maji...

5. Kunywa maziwa yasio na mafuta (skim milk, fat free milk)

6. Jitahidi kupika kwa njia nyingine badala ya kukaa bha kama baking , broiling, microwaving na poaching.

7. Ukiwa unanunua chakula kama vina label tafuta vyakula vilivyoandikwa no sugar added au hata kama vimeandikwa diabetics. Ni muhimu kusoma label kama vyakula hivyo vimeandikwa.

8. Badala ya kutumia chumvi tumia viungo mabali mabali kuweka ladha kwenye chakula chako.

9. Jaribu kutafuta vitafunio vyenye virutumisho. Ni heri ule bag la low fat pop corn kuliko kula kipande cha cake. Na ni heri ule chungwa badala ya kunywa orange juice.