Wednesday, August 10, 2011

Dalili za Shinikizo la juu la damu

Mara nyingi BP haina dalili ndio maana inaitwa silence killer. Mpaka upime pressure yako ndio utajua iko juu. Lakini wale wenye BP ambayo ipo juu sana dalili zao ni kama kuumwa kicha, kichefuchefu, kutapika, kizunguzungu na kuona maruwe ruwe. Lakini watu wanaoona dalili hizi ni kuwa BP yao imeshafikia juu sana na hapo ni hatari kwa maisha yao.

Watu wengi hawendi kupata matibabu mpaka BP iwe imeshaharibiu viungo vya ndani vya mwili.

Viungo vya ndani ya mwili ambavyo mara nyingi huharibiwa na High BP ni kama Heart Attach, kufeli kwa moyo, kufeli kwa maini, kiharusi, macho kuharibika na mguu kuuma.

Na High BP inaweza usijue unayo kwa muda mrefu au mpaka iharibu viungo vya mwili ndio mtu anakimbilia kutafuta matibabu.