Jifunze Kuongea Kiingereza.
Kitabu cha kujifunza kuongea Kiingereza kitapatikana hivi karibuni. Kitabu hiki nimeanza kukiandika kama miaka 6 iliyopita. Hii ni baada ya kuona ni jinsi gani watanzania wengi wanajifunza shuleni kiingereza lakini bado inakua vigumu kuongea au kusikia mtu akiongea kwa kiingereza.
Mimi sikusoma elimu ya msingi shule za "ST " au "Academy". Shule ambazo zilikuwapo wakati nasoma bali zilikua nje ya uwezo wa wazazi wangu ni Arusha School, St Augustine na Kilimanjaro International School. Pamoja na kuwa nilisoma mpaka form six Tanzania na nilikua kati ya wanafunzi tuliokua tunafanya vizuri (academically) lakini hiyo yote haikuweza kunisaidia kujua kuongea Kiingereza bila kuwa na uoga fulani au kutokueleweka. Tatatizo hili lipo kwa wengi mpaka sasa kwa wale wanaosoma za serikali Tanzania.
Baada ya kuangalia ni kwanini tunajifunza kiingereza toka darasa la tatu lakini bado hatuwezi kuongea au kusikia watu wanaoongea kiingereza kwa ufasaha nikagunduua ni jinsi gani tunavyofundishwa na ni jinsi gani tunastahili kufundishwa. Kuna sheria nyingi za kingereza ambazo mwanafunzi anatakiwa kuzijua ambazo hatufundishwi. Kuna tofauti ya kutamka lugha mbalimbali ambazo hatuambiwi wakati tunapofundishwa hivyo wengi hufukiria au huongea kiingereza kwa kutumia sheira za lugha ya kiswahili....
Lugha ya kiingerea ni lugha zinazojulika kuwa kati ya lugha rahisi kujifunza. Wataalamu wanasema inahitaji masaa 600 tu kuweza kuongea kabisa Kiingereza. Hivyo nilianza kuangalia jinsi wanavyofundisha watoto na pia wale wanaosoma English as a second language. Kitabu changu pia ni baada ya kujifunza lugha tatu (spanish, german na french) na kuangalia wao wanafundisha vipi hizi lugha kwa watu wengine? Nini tofauti ya hizi lugha na kiingereza? Hivyo kitabu changu kitaweza kukufundisha kuongea Kiingereza kwa waswahili wengi. Kitabu hiki kimetengenezwa kwa kufuata kiinereza cha wamarekani. Ila ukishaweza kuongea kiingereza cha marekani hata kiingereza cha waingereza au waaustralia utaongea bila matatizo.
Utaelewa siri mbalimbali wanazotumia walimu wanaofundisha wanafunzi hapa wasioongea kingereza. Ni nini kitakusaidia wewe kuongea na kusikia kiingereza mapema. Ni ini kitakusaidia kuongeza speed ya kiingereza unachoongea haraka. Ni nini kinakukwamisha kuongea kiingereza kwa ufasaha...
Kwanini ujifunze kuongea Kiingereza?
Kujiamini - Ukiweza kuongea kiingereza utaweza kujiamini zaidi.
Ajira - ukiweza kuongea kiingereza utaweza kupata ajira mbalimbali. Hivyo nafasi yako ya kupta ajira inamshinda yule asiyeongea kiingereza.
Kupandishwa cheo - Ukiweza kuongea kiingereza utaweza kupandishwa cheo haraka kuliko yule asiyeongea kiingereza
Safari nchi za nje - Kila mahali unapokwenda katika nchi mbali mbali utakuta kuna watu wanaoweza kuongea kiingereza na sio lugha nyingine kuu za ulimwengu huu. Hivyo kwa kujua kiingerreza utaweza kusaidiwa au kuwasiliana kwa urahisi na watu.
Biashara - Ulimwengu unazidi kuwa mdogo kila siku. Sio lazima uwe nje ya nchi. Hata kama unafana biashara ndani ya nchi au online ni lazima utakutana na wateja wa nchi nyingine ambao watataka kuongea na wewe kwa kiingereza. Ufanisi wako wa kuongea kiingereza utaweza kukuongeze wateja na faida katika biashara yako.
Ongezeko la faida - Ukijua kuongea kiingereza utapunguza gharama a kuajiri watu wakuangalia documents zako za biashara au kutafuta washauri wanaoongea lugha ya kiingereza unapotaka kufanya mikataba mbalimbali.