Picha kutoka envaya.org |
Kwa kuweka hilo bila kuweka umri kamili wa mtoto ni kusafisha mikono yao lakini kiukweli ni kuacha kumlinda mtoto huyo na kuiachia sheria za mila na jadi ziendelee. Kumbuka kila kuna makabila mpaka leo yanayowaachisha sule wanafuzi wa kike ili waolewe mara wakifikisha umri wa mika 12. Je hao wasichana mtetezi wao ni yupi? Ni muhimu sana kuweka umri halali wa mtoto wa Tanzania.
Jambo lingine nililokua nafikiria ikiwa hii katiba itapita basi sheria ya kusimamisha wanafunzi wakipata mimba itakua ni against the law. Kama mtoto ana haki ya kupata elimu basi regardless ya jambo lolote litakalomkuta katika maisha yake, haki yake ya kupata elimu bado ipo. Kama serikali inasema mtoto ana haki ya kupata elimu na wakati huo huo serikali hiyo inawaachisha tena watoto hao shule mara watakapopata mimba katika shule za serikali. Je huo sio upungufu wa kufikiri, unafiki, na kufuata sheria za mila, jadi na dini? Kama ni shule za private wakifanya hivyo ni sawa kwa vile ni mtu akienda shule hizo anatakiwa kufuata sheria zao lakini kama ni shule za serikali hiyo sio halali kabisa.
Na pia wakishaweka umri halali wa mtoto (nchi nyingi ni chini ya miaka 18) sasa kama mwanafunzi alichelewa kwenda shule ana kujikuta bado yupo shule akiwa na umri wa miaka 18 ni kwanini naye afukuzwe akipata mimba? Je yeye si mtu mzima na ana haki ya kujiamulia analofanya? Kwa kufukuza shule katika shule za serikali ni mapungufu katika sheria za Tanzania. Na hii yote ni kwa wanaume wanaotengeneza sheria hizo bila kujali kuwa wanaowapa mimba wanafunzi hao ni wanaume.
Ninasikitika sana nikiona wasichana wengi wanaachishwa shule wakipata mimba. Ndio sio vizuri kwa jamii lakini jambo hili ni moral issue na linahitajika liwekwe kwenye kusaidia jamii kuelewa kwa nini wasichana wengi wanapata mimba wakiwa bado mashuleni? Kuwaachisha shule tu bila kujadili jamii ni upungufu wa kutafuta short cuts. Ni kufikiria kwa kufanya hivyo ndio kupunguza tatizo hilo.
Kwanza inasemekana kuwa watoto wengi wanaopata mimba mapema wametoka katika nyumba ambazo ni mama au baba peke yake tu anatunza familia (Single parent home). Pia wanasema wale wanaotunzwa na bibi na babu chance ya kupata mimba ni kubwa kuliko wale wanaotunwa na wazazi wake. halafu pia kuna ushahidi kuwa watoto wanaopata mimba wazazi wao ni walevi sana, mzai mmoja ni muhuni (baba au mama), au baba anamtesa sana mama yake. Hivyo kukimbilia kufukuza watoto wakipata mimba bila kutafuta kiini cha tatizo hilo halitapunguza tatizo hilo kabisa.
Pili tukumbuke kuwa “When you educate a man; you educate a man. When you educate a woman; you educate a generation.”- Brigham Young. Mwanamke anayeelimika chance ya mtoto wake kutokufa mapema ni kubwa kwa vile anakua anajua umuhimu wa lishe bora. Mwanamke anayeelimika chance ya mtoto wake kupata elimu ni kubwa kuliko yule asiyeelimika. Mwanamke anayeelimika chance ya kuweza kupata kazi na kutunza mtoto wake ni kuwa. Mwanamke anayeelimika itasaidia kupunguza tatizo kubwa sanalinaloikabili nchi sasa hivi ya watoto wa mitaani.
Wakati mwingine huwa naffikiria hao wanwakae viongozi mbona wako kimya tu. Je wao kwanini hawafikirii kutetea maslahi ya wanawake Tanzania? Kwanini hakuna kiongozi aliyejitolea kuichallenge hii law kwa mika yote hii? A wanafikira wao hayo hayatawakuta hata siku moja au kwavile wana hela za kuficha siri? Hivi nani hajaona mwanafunzi aliyepata mimba aliyetokea katika familia yenye jina kubwa mara akahamishwa shule? Mara anaenda shule nyingine fresh kama hakuna kitu kilichotokea bali wameficha mtoto.
Sio kila mtu ana hela za kuficha siri, kuhamisha mtoto kwenda shule nyingine au kuwapeleka watoto hao nje ya nchi wakamalizie masomo. Na hata siri ikiweza kufichwa lakini je ni behavior issues gani wanazokua nazo hao watoto mara wanapojua kuwa mtu anayekuwa anamuita mama ni bibi yake na yule anayekuwa anamuita dada ni mama yake? Wengi tumewaona wanaishia kuanza kuwa walevi, kuvuta bangi, kuwa wahuni na mwishowe kuacha shule. Je nani wa kulaumiwa hapa? Jamii a serikali?
Inabidi tubadilike kwa vile unafiki hautaisaida nchi chochote zaidi ya kurudisha nchi nyumba.