Friday, December 09, 2011

Miaka 50 Ya Uhuru wa Tanganyika - "TUNAWEZA"

Leo ni miaka 50 imepita toka Tanganyika ijipatie uhuru wake. Kama nchi nyigine ulimwenguni kote  tunajua kuwa kuna mazuri mengi ya kufurahia katika siku hii na kuna mabaya mengi ya kusikitisha tukitafakari katika siku hii. 

Nimekaa nikawa nafikiria watu walitetea kupata uhuru wetu je siku hiyo walivyoupata walijisikiaje? Je walifurahia vipi? Na machoni kwao walikua wanafikiria Tanganyika katika miaka 50 itakuaje baada ya kumwondoa mkoloni? Waliohangaikia huu uhuru siku hiyo kama wengine bado wapo hai leo katika miaka hii 50, maisha ya watu yalivyo sasa hivi na nchi ilivyo kwa ujumla je ndio jinsi walivyotarajia? 


Nilikua naangalia show moja ilikua inazungumzia nchi ya Estonia ambayo ilijipatia uhuru wake 1991. Mwaka 1992 inflation ilikua 1000%. Unemployment ilikua 70%. Kulikua hakuna magari barabarani kwa vile kulikua hakuna gasoline. Kazi zilikua hakuna kabisa lakini sasa hivi Estonia ni moja ya nchi za Europe ambazo uchumi wake umekua sana na bado uchumi huo unakua kwa kasi kubwa sana...Kiongozi huyo alivyokua anahojiwa maneno yake yalinifurahisha na nilijifunza vitu vingi sana. Je ni nini wamekifanya kufikia hapo?

Hivyo leo kwa kusherekea miaka 50 ya uhuru nimeamua kuanzisha topic katika blog hii ambayo itakua inazungumzia mambo mbali mbali. Ni jinsi gani nchi nyingine zimeweza kufikia hapo zilipo? Katika pitia pitia blog nyingi za Tanzania jina la blog ya Evarist Chahali "Kulikoni Ughaibini" lilinivutia. Na maana ya hil jina ilinivutia sanal Kwanni sisi kwetu tusiweze? Wao huko ughaibuni wana nini cha zaidi? Kulikoni Ughaibuni mpaka wao waweze kufikia hapo walipo?  

Sasa kwa vile tunajua watu wengi na hata viongozi na wananchi wengi wanasoma tweets na blogs hivyo ni heri kuwaeleza na kujifahamisha sisi wenyewe ni nini tofauti yetu na ya nchi zilizofikia hapo zilipo. Labda wakati mwingine hatuoni au kuelewa ni nini kifanyike au wenzetu wanafanyaje?. Tunafahamu viongozi na wananchi wengi wanasoma tweets na blogs basi ni heri tuelezane ukweli au tufahamishane.. Hii ni kwa ajili ya kujenga na si kwa ajili ya kubomoa. Mafisadi live them alone here. Tuangalie ni nini kikifanyika ili tuweze kujikomboa katika maisha?..Ukiangalia wengine wamepata uhuru chini ya miaka 20 lakini maisha yamebadilika na kuwa mazuir mara 200% kwa nini sisi miaka 50 ya uhuru lakini mpaka sasa nchi iko hivyo?  

Hivyo ideas mbalimbali zinakaribishwa..Jina na credits zinatolewa kwa mtu anayetuma na post yake kupostiwa.  Hash tag TUNAWEZA

No comments: