Kuna siku niliuliza swali hili kwenye twitter "Je ni wanafunzi wangapi waliomaliza elimu yao ya juu nchini Tanzania wameshawahi kutafuta kazi nje ya nchi (East Africa) baada ya masomo yao? Well, sijapata hata mtu mmoja aliyejibu mpaka sasa hivi hata kusema mimi nilijaribu lakini sikupata. Sasa sielewi ni kuwa hakuna mtu aliyewahi kutafuta kazi nje ya nchi baada ya masomo yao ama?
Sikuuliza swali langu kwa kebehi ila tu kwa kutaka tuelimishane.Ila baada ya kusubiri kwa muda mrefu bila jibu maswali mengine yamenijia kichwaji. Je elimu ya Tanzania sio nzuri kuweza kushindana katika soko la ulimwengu? Je elimu ya Tanzania haifundishi kumwandaa mwanafunzi kuweza kufanya kazi mahali popote ulimwenguni? Je ni wanafunzi wenyewe hawajiamini kujaribu kutafuta kazi nje ya nchi? Je utamaduni wetu ndio unawafanya watu wasiwe na mawazo ya kutafuta kazi nje ya nchi baada ya masomo yao kwa kufikiria kukimbilia nje ya nchi ni kutoipenda nchi yako?

Nakumbuka kipindi nikiwa college viongozi wengi kutoka Tanzania walikua wakifanya mikutano na watanzania walikua wanasema "vijana mkimaliza masomo yenu mkumbuke kurudi nyumbani kulijenga taifa". Watu walikua wanawauliza turudi nyumbani kazi zipo wapi? Waliomaliza tu nchini wengi hawana kazi. Lakini siku hizi katika mikutano mingi nimegundua kuwa kauli yao imebadilika. Wengi huwa wanasema "Vijana mkumbuke kuwekeza nyumbani" Na mikutano ya Diaspora ndio ikaanzia hapo. Kila investor anakuja kupitch agenda zake za jinsi ya kuinverst Tanzania. Naona wamegunduka siku hizi kulijenga taifa sio lazima mtu aishi Tanzania.
Sasa turudi nyuma kwenye the reality check ya maisha. Mimi nimefanya kazi na baadhi ya watu kutoka India, Ghana na Philippines ambao wao hawakupata elimu yeyote hapa USA bali wamekuja kufanya kazi tu kwa kutumia visa za kazi. Na katika kuongea nao hakuna hata mmoja aliyeniambia alitafutiwa kazi na ndugu yake au mtu fulani anaye mfahamu. Ila kuna baadhi ambao recruiters walikwenda huko kwao hao tuwaache pembeni. Wengine wote ambao hawakuwa na recruitment program yeyote wametafuta online na kuapply wenyewe. Sasa nikiona hivyo najiuliza kwanini watanzania nao hawana tabia ya kutafuta kazi na kuapply nje ya nchi? Kwanini sisi tuwe na mawazo ya kuwa sio vizuri kupata elimu Tanzania na kwenda kupata ajira nchi nyingine kama kazi hazipo za kutosha?Kwanini tufikirie tu kuwa nje ya nchi ni kwenda kusoma tu?
Hivi hao wahindi, wachina, wakenya na wanigeria hapo Tanzania wanaofanya kazi mnafikiria hawapendi kwao? Ukipitia baadhi ya blogs comments unazoziona unafikiria hivi huyu anayesema hivi anaelewa anachokisema kweli? Hakuna mtu asiyependa nyumbani kwao lakini kama myumbani hakuna kazi inabidi mtu uanze kufikiria sehemu nyingine. Na kufanya hivyo haitakupunguzia uzalendo wa nchi yako. .
Kila siku nawaambia watu ukweli kuwa sio kila anayeishi nje ya nchi ana maisha mazuri kuliko wanaoishi Tanzania. La hasha kazi za huku kwanza ukilinganisha na Tanzania uwajibikaji wake ni tofauti sana. Ukizembea huna kazi na anapewa mwingine, bali kama mtu hana kazi na maisha hayaendi kama ulivyotegemea ni bora kutafuta kazi nchi nyingine. Huwezi jua ni nchi gani inahitaji ujuzi ulio nao. Na sio kuwa nasema kila anayemaliza shule basi akimbilie kutafuta kazi nje ya nchi hapana kuna watu bado elimu zao zina ajira Tanzania ila kwa wale ambao masomo yao waliyosoma kazi ni chache basi ukiwa unatafuta tafuta kazi iwe sambamba ndani na nje ya nchi. Katika muda wako jifunze kutengeneza CV/Resume zako kwa syle ya nchi tofauti ukiona kazi appy. Na uwe mkweli toka mwanzo usidanganye kuwa unaishi hiyo nchi kazi ilipo ukitegemea utaenda tafuta tourist visa uingie halafu ndio ukumbane nao huko kwa huko, hapana waeleze ukweli toka mwanzo.
Internet zimefungua ulimwengu sasa ukiitumia vizuri huwezi jua bahati yako iko wapi? Ila ukweli ni kuwa usijidanganye kwenda nchi yeyote na visa ya kutalii au kama umeforge kuwa wewe ni mfanya biashara mkubwa huko Tanzania halafu ufikirie utaweza pata kazi ukisha ingia kwenye hiyo nchi. Kama ni umesoma professional kama medicine, umefanya accounting na kumaliza CPA kabisa, ama law utaharibu sana elimu yako uliyoisoma Tanzania..Hilo ni kosa kubwa sana sana ukisikia kuwa dr analipwa kwa saa $250 halafu ukimbilie kuingia USA ukifikiria utakubaliwa kufanya kazi na kupata hiyo hela. Ukifanya hivyo utaishia kujilamu. Kuna wengi tumewaona wamengia sasa sijui walikua hawana ufahamu wowote au ni ile ya kudanganyana kazi ziko nyingi sana katika career fulani hivyo nikienda huko kitu cha kwanza asubuhi ni kuamkia kazini. No way....Kuna watu wana degree za medicine, wengine wana CPA za Tanzania na wako mitaani na hawawezi kufanya kazi katika field zao. Tatizo ni kuwa hawakuelewa ukiritimba wa hizo field. Ila pia wako wengi madoctor wengi tu ambao hawakusomea hapa lakini walijua nini cha kufanya kabla hawajaingia huku, wakajitayarisha vizuri na kufuata sheria za kazi hizo.
Honesty uchumi ulivyovurunda sasa hivi lakini kuna majors ambazo bado zinachukua hata watu walio nje ya nchi na software engineering ni moja wapo. Pia kuna siku nilisoma gazeti walikua wanahitaji pharmacists kwenye zile states ambazo wamarekani wenyewe hawataki kwenda kuishi huko. Huwezi jua unachokijua kinahitajika nchi nyingine kwa kiasi gani. Ndio maana hapa wazungu wanajitahidi sana kuwasomesha watoto wao kichina wakijua kuwa huko kesho itakuwa kwa wenzao uchumi umepanda sasa watoto wao watakua wamejiandaa vipi? Sasa watanzania pamoja na masoko hayo je tuko tayari kiasi gani katika hili soko la kimataifa? Curriculums zimetengenezwa vipi ili kuweza kuandaa mwanafunzi kuweza kufanya kazi mahali popote ulimwenguni? Mambo ya kufikiria nikienda fanya kazi nje ya nchi basi siipendi nchi yangu au ndio nimeikana naona hayaendani na ukweli wa maisha. Lets be honest...

No comments:
Post a Comment