Thursday, October 20, 2011

Mambo mengine yasijadiliwe katika katiba mpya ya Tanzania

Nimeona hii tittle kwenye blogs kadhaa zimeandika "Wasomi wa Tanganyika wasema katiba ya Muungano isi jadili Muungano" Kwanza nilijiuliza ni wasomi wangapi? Na kigezo cha mtu kuitwa msomi ni kipi? Na kwa nini mtu achukue mawazo ya mtu mmoja na kuyajumuisha kama ni ya wasomi wote? Kwa upande wangu kuandika kama hivyo ni kuudanganya umma. 

Maoni ya mtu mmoja sio ya kujumlisha kama ni ya wasomi wote nchini. Ukishaanza kusema hivyo basi wale ambao sio "wasomi" wataanza kurudi nyuma na kujiuliza maswali mengi...Kama wanaiotwa wasomi wanasema hivi je mimi nisiyemsomi nikisema nitasikilizwa? Mimi siyesoma ninajua nini? 

Kwanza kabla ya kumshabikia huyo aliyetoa mapendekezo yake hayo tunaomba watuambie ni sababu gani zimemfanya afikie hilo? Anasema tu hayo ni mambo nyeti...Je mambo nyeti ni yapi? Kwanini kila siku mambo nyeti yanayohusu huu muungano hayawekwi hadharani tukayajua na kuona faida au hasara zake? Na kama katiba ni mpya ya Tanzania kwanini ijadili  mambo machache na mengine  isiyaguse? Je hii katiba mpya ni kwa manufaa ya wote au wachache tu? Kwa nini wachague mengine ya kubadilisha na kuongelewa na  mengine yasiguswe?

Halafu kingine huwa nashangaa ni jinsi watu wazee wanavyo utreat huu umoja wa Tanganyika na Zanzibar kama yai vile. Kitu kidogo msiongee hili litavunja umoja. Kitu kidogo hayo ni mambo nyeti msiyaguse..Kila kitu kina umuhimu kwa wakati uliopo. Si ajabu huo umoja ulipoanzishwa miaka hiyo ulikua una manufaa je wakati huu wa sasa manufaa yake bado yapo? Kama yapo mnaweza kutwambia? Je wameshauliza upande wa bara watu wanaona vipi kuhusu huu muungano au wanapata faida gani na huu muungano? Je huko upande wa Zanzibar wanachi wameshaulizwa hayo maswali pia? 

Watu wanasahau kuwa nchi inaundwa na wananchi sasa kama mtu ataamua kuwalazimisha wananchi kuishi kwa matakwa yake haitakua busara kufanya hivyo. Mwananchi awe msomi au asiwe msomi katika kila jambo linalohusu nchi ni vizuri kushirikisha watu wote bila kujali jinsia, umri, kabila, siasa, elimu wala dini. Views za watu wote ni muhimu kuzithamini ili nchi iwe na amani. KIla mtu anaruhusiwa kusema lakini isiwe kigezo cha kulable maoni yake kuwa ni kutoka kwa wasomi Tanganyika..That is just wrong...

Miaka ya nyuma kulikua na umoja wa East Africa lakini haukudumu na ulivunjika kwa vile wakati huo kulikua hauna manufaa. Sasa hivi unarudi tena labda sasa hivi ndio wakati wake au ni kwa wachache tu wanataka kwa masilahi yao time will tell.... Je bila kurekebisha sheria zote hata zinazohusu huu umoja itakua ni katiba mpya au ni vipengele baadhi tu ndio vinarekebishwa? Kama katiba itaitwa mpya basi izungumzie mambo yote yawe yanakwenda na wakati na sio machache tu kwa manufaa ya wachache....