Wednesday, October 12, 2011

Vyakula vya kusaidia uso wako kung'aa

Nuru na ngozi inayong'aa iko kwenye wish list ya mwanamke. Kila mwanamke anapenda ngozi yake iwe na sura ya ujana na inayong'aa kila siku. Watu wengine wanafikiri cream la lotion za gharama ndio zitawasaidia kuuweka ngozi iwe katika hali hiyo forever. Je unajua jinsi ya kukeep ngozi yako katika hali ya kung'aa bila kupoteza hela nyingi katika cream ambazo mara nyingi huwa hazifanyi kazi? Mlo wako unaokula kila siku unachangia sana ngozi yako kuwa inang'aa au kufifia.Vitu vya kuzingatia katika mlo wako kila siku ni hivi:-

Mafuta
Ingawaje unajitahidi kupunguza uzito au kumaintaine uzito ulionao lakini uso wako ni sehemu ya mwili ambayo inahitaji mafuta zaidi. Kula milo yenye mafuta yenye afya kitakusaidia kuweka ngozi yako. Monounsaturated oil huwa inapatikana kutoka kwenye vyakula kama maparachichi, nuts na olive oil.


Omega 3  fatty acid
Samaki huwa zinasemekana ni nzuri kwa kwa moyo na  kukusaidia katika brain lakini pia omega 3 fatty acidi ni nzuri kwa kuweka ngzi yako iwe soft na smooth. 

Vitamin A
Jitahidi kula vyakula vyenye vitamini A. Vitamin A inasaindia kuondoa wrinkles au fine lines. Vitamin A inapatikana katika vyakula vyenye rangi ya orange kama mapapai, cantaloupe au carrots.

Vitamin C
Vitamini C inapatikana kutoka kwenye vyakula kama Citrus fruits, mananasi, pilipili hoho, broccoli, strawberries na kiwi 

Biotin
Biotin ni vitamin B ambayo inapatikana kwa wingi kutoka kwenye kiini cha yai na maini

Zinc
Zinc inasaidia ngozi iliyoharibika na pia inasaidia kundoa chunusi. Inapatikana kwa wingi kutoka kwenye vyakula kama oyster, crabs, wheat germ, ndizi, lean beef, sesame seeds, pumpkin au squash seeds, dark chocolate, nyama ya kondoo na karanga

Non refined cards diet
Starch kwa watu wengine wakila inawaletea chunusi chunusi lakini pia ukila starch kwa muda mrefu itaacha ngozi yako iwe saggy. Hivyo jitahidi ule nafaka ambazo hazijakobolewa.

Maji 
Kunywa maji kwa wingi pia inasaidia sana ngozi yako iwe inang'aa.
 
Mazoezi
Jitahidi sana uwe unafanya mazoezi ili damu itembee mwilni vizuri. 

Jua
Jitahidi sana kukaa kukinga ngozi yako isipate direct sunlight kwa wingi. 

Stress
Stress zinaharibu ngozi. Jitahidi uwe unaweza kumanage stress zako.

Kulala
Hakikisha unaweza kulala kwa masaa 6 hadi 8 kila siku.