Jumamosi iliyopita nilikwenda kwa local farmers market. Farmers markets huwa wakulima wako very friendly na wengi huwa wanapenda kuelezea mazao yao na mambo mengine mbalimbali. Katika pita pita huku nikiongea na watu mbalimbali mara nikakutana na mdada mmoja ambaye baada ya kuongea aliniambia kuwa alikua Tanzania kwa kipindi cha miaka miwili.
Nilifurahi kuona na yeye alifurahi sana alivyofahamu nimetokea Tanzania. Katika mambo tuliyoongea jambo moja liliingia kichwani alipokua anaelezea kuwa muuza magazeti hapo alipokua ananunua gazeti kila siku alikua anamshangaa kuwa yeyey ni mwanamke na iweje awe ananunua gazeti? Akaniuliza ni jadi yetu kwa wanawake kutokununua newspapers? Mimi nilimwambia kuwa huwa tunasikiliza news just not the paper.
Well, nilivyorudi nyumbani nilipata flash back nikakumbuka nyumbani kwetu mama alikua hana tabia ya kununua newspapers pia. Ilikua kama baba hatakwenda mjini basi ndio atamtuma mama akirudi nyumbani aje na newspapers. Na akileta newspapers wala hatafungua kusoma na kama akisoma ni page ya kwanza tu basi. Ilikua baba anasoma na kama kuna jambo la maana ndio ataaanza kutuelezea. Nilivyoanza kujifunza kusoma ndio mimi kati ya wasichana watatu nyumbani ndio nilikua napenda kusoma sana newspapers. Nilikua nasoma newspapers from page one to the last page. Ila baba alikua akisafiri kutaua hakuna newspapers mpaka akirudi.
Lakini serious je ni kwanini? Je ni kwa vile jadi yetu ilikua wanaume ndio wanapelekwa shule na wanawake elimu ilikua sio ya kwao? Je ni kufikiria kuwa newspapers ni kwa wanaume tu? Je nikutopenda kuwa na ufahamu wa mambo mbalimbali yanayotokea nchini au ulimwenguni? Je ni kwa vile wengi huwa wana uvivu wa kusoma na hupenda kuhadithiwa yaliyotukia au ni lingine? Au ni kufikiria yanayotokea hayatuhusu sisi wanawake?
Hebu jiulize mwenyewe kama wewe ni mwanamke. Siku hizi news sio lazima kuzipata kwenye papers lakini je kitu cha kwanza unachosoma kwenye internet kila siku ni nini? Je habari mbalimbali umezipata saa ngapi? Je priority ya news wewe kwako kila siku ni ya ngapi?