Kitabu changu Jifunze Kuongea Kiingereza - Sarufi sasa kinapatikana Amazon. Kujifunza sarufi za lugha yeyote ile hakuna mwisho ila inakuongezea ufahamu wa kuongea lugha hiyo kwa ufasaha na kujiamini. Nimetumia miaka zaidi ya mitano kuandika kitabu hiki na nimejifunza mambo mengi sana nilipokua nafanya utafiti wa mambo mbalimbali katika kukamilisha kitabu hiki. Nimejitahidi sana kuandika mambo hayo kwa ufupi na kutoa mifano mingi kuliko maelezo ili kufanya msomaji aweze kuelewa zaidi.
Katika kitabu hizi nimegusa mambo yote kuanzia familia za maneno, vibainishi, viwakilishi, ujenzi wa sentensi, vituo vya uandishi na mambo mengine mengi ambayo yatakusaidia kuweza kuwasiliana katika lugha ya Kiingereza bila kuwa na makosa mengi. Jipatie kitabu hiki ujifunze Kiingereza kwa gharama ndogo sana, kwa muda wako na nyumbani kwako.