Kila siku studies mbalimbali zinatoka kuhusu madhara ya mionzi iliyonayo simu za mikononi na simu ambazo hazina code. Je umeshakaa ukafuatilia hizi studies? Kuna mambo mengi watu wanakua wanafichwa au wenye makampuni hayo hawasemi ukweli mpaka ikishafikia watu wengi wamepata madhara ndio ukweli unaelezwa.
Leo nimeona study nyingine iliyokua inafuatilia watu kadhaa kwa miaka kumi ambao ni watumiaji wa simu za mikonomi na wameona 33% ya watu hao wameopata Cancer ya ubongo. Ingawaj study hiyo haijaweza kuunganisha mahusiano yaliyopo kati ya cancer hizo na simu za mikononi lakini ni wakati wetu kuanza kujitahadhari au kuwafundisha watoto wadogo jinsi ya kuwa waangalifu wanapotumia simu za mikononi mpaka hapo ukweli utakapo patikana.
Makampuni mengi hayataki kueleza au kuweka taadhari katika simu lakini ukweli ni kuwa miozi ya simu ni kama vile ya microwave sasa ni kiasi gani ambacho kitamdhuru mtu akikipata kwa siku akiwa anatumia simu hizi au zisizo na mikanda ndio hapo haijulikani. Lakini ukweli ni kuwa kuna madhara fulani yanayotokana na utumiaji wa hizi simu.
Ila dakitari mmoja amesema kuwa kuwaambia watu waache kutumia simu za mikononi ni kitu ambacho hakitawezekana. Ila madhara ya simu za mikononi yanaweza kufikia sawa kama madhara ya kuvuta sigara, asbestos, lead au dawa za kuua wadudu.
Sasa cha muhimu ni heri kuchukua tahadhari mpaka hapo utafiti wa kisayansi utakapopatikana
Mambo madogo dogo ambayo yataweza kukusaidia kupunguza hii miozi ni kama:-
1. Unapotumia simu jaribu kuiweka kama 3.4 inches kutoka kwenye sikio
2. Jitahidi kutumia headphones muda wote unapotumia simu
3. Tumia speaker phone.
4. Text zaidi kuliko unavyotumia simu yako kwa maongezi.
5. Jitahidi usitumie muda mwingi kwenye simu kama umeiweka kwenye sikio
6. Jitahid kuiweka mbali na reproduction organs zako hasa kwa wanaume ambao hawajapata watoto.
7. Jitahidi usiweka simu hiyo karibu na mifupa (Wengi hupenda kuweka simu mfukoni au kwenye clip) Hiyo sio vizuri weka kwenye pouch au bagi ya mgongoni.
8. Jitahidi kutowapa watoto wadogo simu waongee nayo kwenye sikio.