Kuna sites ambazo ukifanya utafiti au kuangalia video clip au viral videos wanakulipa.
Cha kufanya ni kupakua app au kuingia kwa tovuti ya kufanya utafiti huo na kujisajili. Ukishajiunga utatumiwa barua pepe na maelekezo mengine ya jinsi ya kufanya ili uweze kulipwa.
Baada ya hapo ukiwa tayari unaingia kwa app au tovuti uliyojiunga na kuanza kujaza tatafiti yako au kuangalia video clip.
Hakikisha ni sites halali za kufanya tafiti hizo. Hazihitaji mtu kulipa hela yeyote ili kujiunga. Ni bure kabisa. Ukiona umeingia kwa site na wanataka uwalipe hela kujiunga, kimbia. Hiyo itakuwa ni site ya utapeli.
Baadhi ya site halali ni hizi:-
Ipsos I-Say. Zinalipa kuanzia $15.
Pinecone Research. Zinalipa kuanzia $1.
Toluna. Zinalipa kuanzia $5.
Inbox Dollars. Zinalipa kuanzia $30.
My Survey. Zinalipa kuanzia $10.
Swagbucks. Zinalipa kuanzia $5.
Point Club. Zinalipa kuanzia $10.
Nielsen Digital Voice. Zinalipa kuanzia $50.