Tuesday, October 01, 2019

Jinsi ya Kutengeneza Serum ya Kutunza Ngozi ya Uso

Serum ni kitu muhimu sana kutumia katika utaratibu wako wa kila siku wa kutunza ngozi yako ya usoni. Hii ni moja ya aina za serum ambazo ninazitumia. Hakikisha hutengenezi nyingi sana kwa mara moja kwa sababu huhitaji kutumia nyingi sana kila siku unapotumia, hivyo kiasi utakachotengeneza inaweza kuwa nyingi sana na kukaa hata mwaka mmoja. Ili iwe na ubora mzuri ni muhimu kutumia kwa miezi sita na siyo zaidi toka ulipoitengeneza. Weka kwenye fridge ambayo huhitaji kutumia kila siku mpaka wakati unapoihitaji. 

Kitu kingine cha kuzingatia ni kuhakikisha kuwa unatumia mafuta ambayo ni bora. Ubora wa mafuta yako unayotumia ndio utakusaidia kufanikisha kupata matokeo mazuri unayohitaji kufikia. 

Hii serum ni ya kupunguza ngozi yako kutokua haraka. (kupigana na uzee). Unatakiwa kutumia mara mbili kwa siku baada ya kuosha uso wako na kutumia toner kama unatumia au kama hutumii toner basi ni kabla ya kupaka moisturizer yako unayotumia kila siku.



Mahitaji 
- Vijiko viwili vya chakula - Mafuta ya Nazi (Organic) 
- Vijiko viwili vya chakula - Mafuta ya Mparachichi (Organic)
- Vijiko viwili vya chakula - Mafuta ya Mizeituni (Organic) 
- Drop nne za mafuta unayoyapenda
- Chupa yako ya kuhifadhia seruma yako.

Jinsi ya kutngeneza
- Yeyusha mafuta ya nazi.

- Weka kipimo chako juu ya meza au kama unatumia vijiko kwa kupimia basi hakikisha unapima sawa sawa.




Changanya vizuri halafu weka harufu yako unayoipenda (Essential oil)


Baada ya hapo weka kwenye chupa zako. |Mimi nimeweza kutengeneza kama 3 ounces. Ambayo hutatumia weka kwenye fridge. Unayotumia weka kwenye sehemu yako unapoweka moisturizer yako au vitu vingine vya usoni.



Tumia tone 2 au 3 tu kabla hujapaka moisture yako. Asubuhi na kabla ya kwenda kulala.
.