Jiandae kununua kitabu changu kipya kitakachokuja mwezi ujao. Jipende ni kitabu kipya cha mambo mbalimbali ya urembo. Kitabu hiki kitawasaidia watu wengi kugundua na kujua siri za urembo bila kuingia gharama nyingi. Unaweza kufikia malengo yako ya urembo bila kuingia gharama nyingi au bila kuingia katika mlango wa saloon yeyote.
Kila mwanamke anahitaji kujiona na kujisikia kuwa yeye ni mrembo. Urembo unaongeza kujiamini. Unapojiamini unafungua milango mingi sana. Unaweza ukawa na elimu lakini ukashindwa kufanya vizuri kwenye interview ya kazi unayoitaka kwavile hujiamini. Kila mwanamke anastahili kujiamini.
Miaka kumi ya kusikiliza na kujifunza kutoka kwa watu waliosomea katika tasnia hii ya urembo. Kila nikienda saloon ya kutengeneza na kutunza nywele wakati nikiwa na natural hair au nimeweka chemicals kwenye nywele zangu au saloon za kutunza ngozi, na watu walionisaindia kupunguza usito baada ya kujifungua. Nimekua nikiuliza maswali mengi na kuandika chini majibu niliyokua ninapewa.
Mambo mengi ni baada ya trials and misses nyingi sana lakini baada ya muda fulani nimegundua kua nimepunguza sana safari na muda niliokua ninatumia kwenda kwenye hizi saloons. Hivyo hela nyingi inabakia kwenye pochi yangu...
Hiki kitabu nimekiandika kwa malengo ya kuwafikia wanawake ila sio vibaya kwa wanaume kuwanunulia wale wapendao. Ni zawadi bora sana itakayowasaidia kupunguza gharama za matumizi ya kwenda kununua urembo.