
Mpaka sasa hivi ninavyoandika hii post nimeshachapisha vitabu vitatu (3) (Modern Swahili, Swahili For Teens & My First Book of Swahili Words) na vingine vinne (4) ambavyo ni (Kids in the Swahili Mom Kitchen, #SwahiliMom Kitchen, East Africa Cook Book & Jifunze Kiingereza) vinakuja hivi karibuni kwa kutumia njia hii hii.
Kabla sijaendela zaidi nataka ufahamu haya:-

2. Kuchapisha kitabu itakugharimu hela sio free. Gharama hizo ni lazima uweke budget ya $300 - $3000 kwa kitabu kimoja. Hizi gharama zinatofautiana kutokana na mahitaji ya mtu na mtu Pia usisahau gharama za kukitangaza kitabu chako. Ni kazi ngumu lakini kama unapenda the reward is priceless. Mimi huwa natumia Guru.com kutafuta vibarua wa kufanya mambo mbalimbali na ndio rahisi kuliko ningeingia kwenye contract na self publishing company yeyote ambazo niliresearch na kuwasiliana nao na wakanipa gharama zao.

4. Hakikisha unaandika topics unazozipenda au unazozijua. Kama hutaenjoy kuandika acha kupoteza muda wako kwavile final product haitakua nzuri. Na pia ikiwa unaandika na hupendi unachofanya hata kama hutapata hela lakini unakua umefurahia rohoni na ukiweza kurudisha hela uliyotumia kutengeneza kitabu chako au zaidi inaongeza furaha yako mara dufu.
inaendelea........